The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Dinna Maningo Mwandishi Aliyechapisha Taarifa za Tuhuma za Aliyekuwa RC Simiyu Akamatwa

Inadaiwa kuwa Maningo amekamatwa kwa kuchapisha taarifa za siri za upelelezi, hata hivyo mpaka jioni ya Juni 15,2024, bado alikuwa mahabusu

subscribe to our newsletter!

Jeshi la polisi linamshilikilia mwandishi na mmiliki wa tovuti ya Dima Online, Bi.Dinna Maningo toka Juni 13,2024. Taarifa kutoka kwa wakili wake zinaeleza kuwa Bi.Maningo anakabiliwa na tuhuma za kuchapisha taarifa za siri za upelelezi.

Itakumbukwa kuwa mnamo Juni 10, 2024, tovuti inayomilikiwa na mwandishi huyu ilikuwa ya kwanza kuchapisha habari kuhusu tuhuma za aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa simiyu. Tuhuma za kumlawiti mwanachuo mmoja jijini Mwanza na kupelekea uteuzi wake kutenguliwa mnamo Juni 11 2024 na Jeshi la Polisi kuthibitisha kumshikilia kwa upelelezi.

Taarifa zinaeleza kuwa Maningo, alikamatwa nyumbani kwake Tarime, mkoani Mara mnamo Juni 13, 2024 saa mbili usiku. Maafisa hao kutoka Jeshi la Polisi walimsafirisha Maningo kuelekea Mwanza, ambako mpaka jioni ya Juni 15,2024, Wakili wake amekuwa akishughulikia suala la kupata dhamana bila mafanikio.

Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Mwanza, Edwin soko ameeleza kuwa chama hicho mkoani hapo ndicho kilichoandaa Wakili baada ya kupata taarifa za kuwasili kwa mwandishi huyo mkoani hapo akitokea Tarime Mara.

“Amefika hapa usiku huu na baada ya kupata taarifa kuwa analetwa Mwanza, tuliandaa mazingira mazuri na mwanasheria yupo naye tayari” alieleza Soko.

Juhudi za kumtafuta kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa bado zinaendelea. Akizungumza na Matukio Daima asubuhi ya Juni 14,2024, Mutafungwa alieleza kuwa hajui uwepo wa taarifa hiyo na kueleza kuwa ataifuatilia kujua undani wake.

Wadau Wazungumza

Tukio hili linakuja ikiwa ni miezi kadhaa tu mara baada ya Mwandishi na Afisa Mahusino wa Chuo cha Michezo cha Malya kilichopo Kwimba mkoani Mwanza kushikiliwa na jeshi la polisi February 23 2024, kwa madai ya kuchapisha habari za uongo kuhusu chuo kikuu cha dodoma (UDOM).

Aidha samamba na hilo, hili linakuwa tukio la tatu kwa waandishi wa Kanda ya Ziwa kupitia kadhia zinazotishia uhuru wa kazi zao ndani ya kipindi cha chini ya miezi sita.

Itakumbukwa kuwa February 20, 2024, mkuu wa wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga, alIkosolewa vikali mara baada ya ya uamuzi wake wa kuwaamuru waandishi wa habari kuondoka kwenye mkutano muhimu, kitu ambacho watetezi wa uhuru wa vyombo vya habari walikosoa vikali.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa taarifa yake kukemea vikali kukamatwa kwa Bi.Dinna Maningo, “Kushikiliwa kwa mwandishi huyu kunaenda kinyume na Katiba na sheria za nchi hii pamoja na misingi ya demokrasia na uhuru wa habari,” ilieleza taarifa hiyo ya LHRC iliyotaka jeshi la polisi kumfikisha Mahakamani au kumuachia huru.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa mara (MRPC) Mugini Jacob, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo June 14, 2024, ameelezea mazingira ya kukamatwa kwa mwandishi huo na kueleza kuwa alikuwa katika hali nzuri alipomtembelea kituoni.

“Tuna imani na jeshi la polisi mkoa wa Mwanza litatoa taarifa sahihi kuhusu tuhuma zinazomkabili mwandishi wa habari Dinna Maningo ili kuondoa sintofahamu iliyojitokeza kwa wanahabari mkoa wa Mara na Mwanza na Tanzania kwa ujumla” alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Juni 14, 2024.

Utafiti wa kitaifa ambao matokeo yake yaliwasilishwa mnamo Februari 16, 2024, jijini Dar es Salaam ulihitimisha kwa kusema kuwa uandishi wa habari ni “taaluma ngumu,” ukionyesha kuwa nusu ya waandishi wa habari kati ya 1,202 waliohojiwa wameripoti kutishwa, kuteswa au kushambuliwa wakati fulani katika maisha yao ya kitaaluma.

Utafiti huo, uliofanywa na Twaweza East Africa ulionesha kuwa waandishi wawili kati ya kumi wamekamatwa au kushikiliwa na mamlaka, na idadi sawa wamepitia unyanyasaji wa kijinsia au kudhulumiwa au vifaa vyao au nyenzo zao kunyang’anywa.

Asilimia hamsini ya waandishi wa habari waliripoti kutishwa, kuteswa au kushambuliwa wakati fulani, huku wengi wao wakisema kwamba maafisa wa serikali ndio chanzo kikuu cha vitisho kwa kazi zao.

Utafiti huo ulibaini kuwa waandishi wengi wanahisi kuwa vyombo vya habari nchini Tanzania vina uhuru mdogo wa kufanya kazi kwa uhuru, bila kudhibitiwa au kuingiliwa na wamiliki wa vyombo vya habari, serikali, watu wenye nguvu na makampuni binafsi.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

19 Responses

  1. Ni vema kuzingatia Sheria za uandishi wa habari ndiyo maana tunasoma. Serikali iangalie upya Sheria za umiliki wa vyombo vya habari especially online tv, kama ilivyo umiliki wa pharmacy, hospitals unavyotolewa kwa wenye taaluma husika tu na iwe hivyo kwa vyombo vya habari. Hii taaluma siku hizi imevamiwa inafanywa na kila MTU kiasi kwamba inaonekana haina thamani. Kuna utofauti wa investigative journalism na udaku. Ni haibu Kwa mwandishi wa habari msomi kufanya uandishi wa udaku (yellow journalism)

    Habari lazima izingatie vigezo vya kuitwa habari (balance of credible, authoritive and eye witness sources) kabla haijaenda kwa umma.

    In this case nina wasiwasi huenda mwandishi pia alitumika kwa maslahi yasiyo ya umma.

    1. Hapa inazungumzwa haki za Waandishi
      Wewe unatuletea Mambo ya Yellow Journalism
      hivi kama ungekuwa ni wewe imekukuta na ukafanyiwa hayo tukae Kimya..? Au tuanze Mambo za Black and Yellow Journalism..?
      Waandishi wa Habari wananyanyaswa mno wanakosa Haki zao kwa Kufumbwa Midomo hasa wanapotoa ukweli kuhusu Watu Maarufu, kifupi inatumika Pesa kuwanyanyasa.
      Waandishi pazeni sauti kutetea Haki zenu achaneni na Chuki kisa aliyetoa ni Wa On line Tv ile hali wewe ni wa News Letter

      1. Kwa hiyo kwakua mna haki kama waandishi, ndo muandike mauongo na kutumika kijinga jinga, halafu Serikali ikae kimya na kuwaangalia tu,, Bro hakuna Taifa linaweza kuendekeza huo upuuzi unaowaza…

    2. Haibu maana yake nini? Au ulitaka kusema aibu? Be careful on what you write, you may end up confusing your audiences.

  2. Ndugu wandishi hizi kalamu mlizoshika ninzuri ila zinapokuwa fimbo za uonevu hapo tunaona,wandishi sikuizi wamekuwa wakitumika kuchafua watu na kuhalibu amani kwa rushwa huchanganya ukweli na uongo,sasa kama tukio hili la RC

    1. Kama alichofanya ni sahihi kwa mujibu wa taratibu za kazi yake basi waandishi wasiwe na hofu atapata haki yake. Sasa kama wana hofu huenda nao hawaamini kama alichokifanya ni sahihi

      Kuna wakati inauma unapoharibu status ya mtu kwa maslahi yako

      Kalamu zitumike kututetea !

  3. Hapa inazungumzwa haki za Waandishi
    Wewe unatuletea Mambo ya Yellow Journalism
    hivi kama ungekuwa ni wewe imekukuta na ukafanyiwa hayo tukae Kimya..? Au tuanze Mambo za Black and Yellow Journalism..?
    Waandishi wa Habari wananyanyaswa mno wanakosa Haki zao kwa Kufumbwa Midomo hasa wanapotoa ukweli kuhusu Watu Maarufu, kifupi inatumika Pesa kuwanyanyasa.
    Waandishi pazeni sauti kutetea Haki zenu achaneni na Chuki kisa aliyetoa ni Wa On line Tv ile hali wewe ni wa News Letter

    1. Wengine tunafikiri kwamba story yenyewe inayotrend na kusugua vichwa vya watu haina mashiko na ishangaza sana. Kwanza nihuyo mdada siyo kwamba amebakwa bali aliyafanya hayo kwa mapenzi yake. Pili huyo dada simtoto mdogo imetajwa Ana miaka 21 na nimwanafunzi wa chuo kikuu. Hatuoni sababu kwayeye kumgeuka mpenzi wake na kumzulia kesi kwa kuwa ni mkuu wa mkoa pengine ilikua kutafuta kujipatia pesa za hila banifu( Black mailing). Watu hununua wasichana ili kuwaharibia wenzao hasa katika mambo ya siasa. Tukumbuke kisa cha mama mmoja aliyetumika kumharibia Mareham Agostino Lyatonga Mrema alipokuwa amejitoa ufahamu na kushinda mtupu mlangoni kwa Mrema akidai kuwa alimtelekeza. Kumbe alikuwa analipwa ili kumchafua mwanasiasa yule. Hata huyu dada na mwandishi wake waliobuni hii story walikuwa na nia tu ya kumharibia sifa huyo mkuu wa mkoa mbele ya Jamii.

  4. Kuna haja ya serikali ,mashirika,na taasisi za kihabari
    Kuwajengea uwezo waandishi wa habari bloggers na wapiga picha kuhusu sheria mbalimbali zinazosimamia tasnia hii ya habari.
    Ninatamani na sisi waandindishi tubalike na tutumie utashi hasa pale tunapotaka kuandika story kuhusu aina ya taarifa . Kwa mfano hizi classified document tunajua kabisa si sheria kupublish taarifa ambazo ni siri bila source.
    Mwisho naomba tukumbuke kuwa ulinzi wa mwandishi huanza na yeye mwenyewe hasa pale unapojaribu kuzingatia taratibu na sheria kuhusu taaluma yako

  5. Subirini tunda likomae ndio Litolewe juu ya mti. Kama alikuwa wa kwanza kupeleka habari hewani au kuichapisha kwenye chombo chake cha habari lazima aisaidie polisi nj jinsi gani aliipata hiyo habari.

  6. Tusubiri tusikie tamko la yule aliyetendewa tendo la kulawitiwa kama amelawitiwa kweli au la. Yeye ndiye shahidi Na. moja.

    Na hawa polisi wanapomkamata huyu Mwandishi aliyetoa ripoti bila shaka wana ushahidi kwamba Mwandishi huyu ametoa habari ambazo ni uzushi mtupu. Lakini kama taarifa ni za kweli, si halali kwa polisi kumsweka ndani na kumnjima dhamana mwandishi huyu. Kwani Mkuu huyu wa Mkoa ni nani hata asikamatwe?

    Mbona mheshimiwa Rais amemtumbua huyo Mkuu wa Mkoa muda mfupi tu baada ya tukio hili kujulikana hadharani?. Kwa nini polisi wasimwambie Raiis kwamba tukio hilo bado halijathibitishwa na kwamba mtuhumiwa yuko huru ili aendelee na majukumu yake?

    Wala mtu asituambie kitu, eti kwamba Mkuu wa Mkoa huyo anaweza akawa ametumbuliwa kwa sababu zingine na sio hii ya kulawiti. Na kama sababu nyingine ipo iweje hatua aliyoichukua Rais ya kutumbuliwa kwake, iende sambamba na muda tukio hili la kulawiti liliporipotiwa na sio kabla?

    Vyombo vya dola viache kuwanyanyasa, kuwaonea, kuwatisha, na hata kuwaua waandishi wa habari.

    Na mamlaka zinazoshughulika na kutetea haki za binadamu wamulike vitendo na hatua zinazochukuliwa na Jeshi la Polisi dhidi ya waandishi wa habari wanapokuwa katika kutimza majumu yao ya kazi kwa haki na uwazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *