The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Undani Kuhusu Mmiliki wa Asilimia 35 ya Kampuni ya Dnata Zanzibar

Nyaraka zinamuonesha  Suleiman Hamad Ali kama mmiliki mkuu wa Maxima Corporation Limited inayomiliki asilimia 35 ya hisa

subscribe to our newsletter!

Dar es Salaam. Maxima Corporation Limited, ndiyo mmiliki wa asilimia 35 ya hisa za kampuni ya Dnata Zanzibar Aviation Services Co. Ltd kampuni inayotoa huduma katika uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume. Wamiliki wanao onekana katika nyaraka za umiliki wa Maxima Corporation ni Suleiman Hamad Ali (51%), Savannah International Zanzibar Ltd (45%), na Sufiyan Aiyub Hafej (4%).

Asilimia 65 zilizobaki za umiliki zinamilikiwa na kampuni yenye makao yake makuu Katika Falme za Kiarabu, Dubai National Air Travel Agency (dnata). Toka kampuni hii ilivyopata kibali cha kufanya kazi zake katika Terminal ya 3 ya uwanja wa Abeid Amani Karume kumekuwa na mjadala usioisha hasa katika namna ilivyopata mkataba wa uendeshaji wa kiwanja cha ndege.

Sheria za uendeshaji wa viwanja vya ndege Tanzania inaitaka kampuni zote zinazotoa huduma katika viwanja vya ndege, isipokua za kujaza mafuta, ziwe zimesajiliwa nchini na pia asilimia 35 ya umiliki wa kampuni hiyo iwe ni Watanzania

Nyaraka za umiliki wa kampuni ambazo The Chanzo imeziona zinamuonesha Ali ambaye ndiye mmiliki mkuu (51%) wa Maxima Corporation yenye umiliki wa asilimia 35 wa Dnata Zanzibar, kama Mtanzania anayeishi Mjini Magharib Unguja.

Jitihada za kumtafuta bwana Ali hazikufua dafu, kwani simu yake iliita bila kupokelewa, tuliambulia patupu pia kwa anuani yake ambayo inaonekana katika nyaraka mbalimbali.

Ripoti yetu inakuja katika kipindi ambapo kumekuwa na majibizano baina ya vyama viwili vinavyounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, huku upande wa upinzani ACT Wazalendo ikitaka majibu juu ya mmiliki wa asilimia 35 za hisa katika kampuni ya Dnata Zanzibar Aviation Services Co. Ltd.

Wamiliki wa kampuni ya Dnata Zanzibar

Wakiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika Nungwi Februari 26,2023, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo alihoji juu ya utendaji wa Dnata katika uwanja wa Abeid Amani Karume, na kuitaka serikali ya Rais Mwinyi kutoa majibu.

Zitto alikosoa uamuzi wa serikali kuzuia watoa huduma wengine kutoa huduma katika uwanja huo (Terminal 3) na kusema ni kinyume cha sheria na taratibu za uendeshaji wa viwanja vya ndege Tanzania na Zanzibar.

“Tunaitaka Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) kuchunguza Dnata Zanzibar Aviation Services Co. Ltd kufahamu ni nani mmiliki wa asilimia 35 za hisa katika kampuni hiyo,” alieleza Zitto Kabwe

“Kwa sababu tumesikia tetesi wakubwa serikalini ndio wanahusika na sisi ACT Wazalendo hatutakubali rushwa ya namna hii kutokea na kukaa kimya” aliongeza.

Rais Mwinyi aliweza kueleza sababu za  serikali yake kutoa ruhusa ya kipekee kwa kampuni ya Dnata kufanya biashara katika uwanja wa ndege wa Amani Karume na kueleza kuwa ACT Wazalendo inasukumwa na maslahi binafsi ya viongozi wake.

Akiongea na waandishi wa habari, Februari 28,2023, Dr Mwinyi alisema kampuni za ndani za kutoa huduma katika viwanja vya ndege  Zanzibar Aviation Services & Travel Trade Ltd (ZAT) na Transworld ziliendesha uwanja kwa miaka 25, hata hivyo serikali iliambulia kupata hasara pekee.

“Sisi awamu ya nane tunaingia, Airport [Abeid Amani Karume] ilikuwa inapata hasara. Serikali ilikuwa inatoa fedha kutoka hazina kupelekea airpot kulipa mishahara. Hizo kampuni wanazozitaka wao. Mwezi uliopita Disemba, robo ya mwisho ile ya mpaka Disemba airport yetu hii imeingiza bilioni 8.1. Kwa robo hii [moja].” Alifafanua Rais Mwinyi.

Hata hivyo Rais Mwinyi hakufafanua zaidi kuhusu hoja za kuipa kampuni ya Dnata ruhusa ya kufanya biashara pekee au kuelezea kuhusu umiliki wa asilimia 35 katika kampuni ya Dnata Zanzibar Aviation Services Co. Ltd.

Akiongea katika mkutano wa hadhara Tibirinzi Pemba Zitto Kabwe alijibu hoja ya Rais Mwinyi kuhusu wao kuwa na maslahi binafsi, “hatuna maslahi yeyote zaidi ya Wazanzibar,” alisema.

Wakati nayaraka mbalimbali zinaonesha Dnata ikimiliki asilimia 65 katika kampuni ya Dnata Zanzibar Aviation Services Co. Ltd, kuna uwezekano kuwa kampuni hiyo ina umiliki wa asilimia 10 katika hisa zinazomilikiwa na kampuni ya Maxima Corporation Limited.

Hii inatokana na taarifa ya mwaka ya Dnata kwa mwaka 2021/22 ambapo katika taarifa hiyo Dnata imeeleza kuwa na umiliki wa asilimia 75 katika kampuni ya Dnata Zanzibar Aviation Services Co. Ltd.

Kampuni moja ya kutoa huduma katika uwanja wa ndege Transworld Aviation iliamua kupeleka malalamiko yake mahakamani, ambapo Januari 17,2023, ilifungua kesi katika mahakama kuu ya Dar es Salaam.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts