The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Watu 13 wamepoteza maisha huku wengine 25 wakijeruhiwa kutokana na ajali ya basi la abiria lenye namba za usajili T178 DVB mali ya kampuni ya Ally’s Star, lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kugonga kichwa cha treni kilichokuwa kikitokea stesheni ya Aghondi kuelekea Manyoni.

Taarifa iliyotolewa na Shirika la Reli Tanzania imesema kuwa kati ya majeruhi 25 wanawake wapo saba na wanaume wapo 18. Na kati ya vifo 13 vilivyotokea wanawake ni sita na wanaume ni saba.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi mkoani Singida chanzo cha ajali hiyo mwendokasi wa dereva wa basi la abiria.

Ajali hii iliyotokea alfajiri ya leo inakuwa ni ya pili katika siku za hivi karibuni kwani Novemba 26, 2023 watu 14 walipoteza maisha kwa ajali ya basi iliyotokea wilayani Tandahimba mkoani Mtwara.

Katika kuelekea mwisho wa mwaka ambapo watu wengi husafiri, wadau mbalimbali wamekuwa wakitoa wito wa wasafiri na madereva kuzingatia sheria za barabarani ili kuepukana na ajali.