The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya mtwara imendelea kusikiliza kesi ya maafisa saba wa polisi wanaotuhumiwa kumuua mfanyabiashara wa madini Mussa Hamis hapa Mtwara.Jana tarehe 27 Novemba 2023 shahidi namba nane wa upande wa mashtaka alitoa ushahidi wake mahakamani hapo.

Hata hivyo mara baada ya shahidi huyo kutoa ushahidi upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa serikali Maternus Marandu uliwasilisha ombi la kuitaka mahakama kupokea hati ya uhalali wa kieleleza cha vipande vya video viwili ili viweze kutumika katika ushahidi wake.

Kutokana na ombi hilo upande wa utetezi unaoongozwa na wakili Majura Magaufu uliweka pingamizi ukitaka ombi hilo lisikubaliwe.

Pingamizi hilo lilizua mvutano wa hoja baina ya pande zote mbili ambapo mara baada ya Jaji Edwin Elias Kakolaki kusikiliza hoja za pande zote mbili alikuja na maamuzi ya kutupilia mbali ombi hilo.

Wakati akitoa maamuzi hayo Jaji Kakolaki alifafanunua kuwa sababu za mahakama kutupilia mbali ombi hilo ni kutokuwa na uhalisia unaoendana na sheria iliyotumika katika kuandaa hati hiyo.

Ambapo alibainisha kuwa upande wa mashtaka ulitumia sheria namba 202 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ambayo hutumika kwa ajili ya picha zilizochapishwa au maandishi na siyo video kama walivyotumia upande wa mashtaka.

Katika kesi hiyo shahidi namba nane wa upande wa mashtaka askari wa jeshi la polisi Nobert Leonard Masawe kutoka polisi makao makuu ndogo ya polisi jijini Dar es salaam kitengo cha kamisheni ya uchunguzi wa kisanyansi ambaye alisema majukumu yake makubwa ni kupiga picha za kihalifu na zisizo za kiuhalifu na kufanya uchunguzi wa kubaini uhalisia wa picha paomja na video mbalimbali zilizorekodiwa.

Akitoa ushahidi mbele ya Jaji Edwin Elias Kakolaki Masawe alisema kuwa mnamno tarehe 22/11/2022, alipata barua yenye maelekezo na flash kutoka kwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Mtwara inayoonyesha video mbili na kutakiwa kuzichunguza kama ni halisi au siyo halisi.

Masawe aliendelea kueleza kuwa baada ya kuzifanyia uchunguzi video hizo alibaini uwepo wa mtiririko wa matukio sawa wa picha na sauti hali inayothibitika kuwa video na sauti ni za halisi baada ya hapo aliandaa hati ya uthibisho wa uhalali wa video hizo na kuzirudisha kwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Mtwara.

Kwa mujibu wa askari huyo , video hizo zilikuwa zinawaonyesha watu wakiitwa kwenye chumba fulani ambapo juu ya meza kulikuwa kumewekwa picha wakiitwa kuzitambua hizo.

Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea kusikilizwa tena siku ya tarehe 28 Novemba , 2028 ambapo shahidi huyo ataendelea kutoa ushahidi wake.