The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Vyama vikuu vya ushirika vya Tandahimba Newala Co-operative Union [TANECU] pamoja Masasi Mtwara Co-operative Union [MAMCU] mkoani hapa leo vimefanya mnada wa tano wa zao la korosho msimu wa mwaka 2023/2024.

Katika mnada huo bei zimeendelea kushuka ambapo kwa chama cha TANECU kilogramu moja ya korosho imeuzwa kwa bei ya juu shilingi 1,900 na bei ya juu shilingi 1755 huku tani 12, 265 zikiuzwa katika mnada huo.

Minada miwili ya iliyopita chama hicho kiliuza korosho kwa bei ya juu ya shilingi 2,035 hadi 1,902 kwa mnada wa nne. Huku ikiuza kwa bei ya juu shilingi 2,150 na bei ya chini shilingi 2,050 katika mnada wa tatu.

Kwa upande wa chama cha MAMCU, katika mnada wa leo kimeuza kilogramu moja ya korosho kwa bei ya juu ya shilingi 1,855 na bei ya chini ya shilingi 1,700 ambapo kimeuza tani 12,773.

Minada miwili iliyopita chama cha MAMCU kiliuza kilo gramu moja ya korosho kwa bei ya juu ya shilingi 2,000 na bei ya chini shilingi 1850 kwa mnada wa nne. Huku nada wa tatu kikiuza kwa bei ya juu ya shilingi 2,135 na bei ya chini shilingi 1,950.

Mpaka sasa vyama hivyo vimeuza zaidi ya tani 106,000 za korosho kwa msimu huu wa mwaka 2023/2024 ambapo bado msimu unaendelea.