Mtwara. Mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miezi 8 ameokotwa leo majira ya asubuhi kwenye ghuba la taka mtaa wa Kiyangu A Manispaa ya Mtwara Mikindani akiwa amefariki.
David George ambaye ni mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo amesema kuwa majira ya asubuhi akiwa anaenda kufanya usafi katika ghuba la taka hilo alimuona mtoto huyo ndipo alifanya taratibu za kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na baadaye kituo cha Polisi.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara ACP Mtaki Kurwijila amethibitisha kutokea kwa kutukio hilo na kusema Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi ili kubaini mhusika na kwa sasa mwili wa kichanga umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Ligula.
Kwa miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na matukio ya aina hii hapa Mtwara kwani mwaka 2022 tukio kama hili liliripotiwa katika kata ya Naliendele na mwaka 2023 kata ya Ligula, Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Imeandaliwa na Omari Mikoma