The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema zoezi la kuwaondoa wakazi wa Ngorongoro ni la hiari na wananchi waepukane na taarifa potofu kuwa kuna uvunjaji wa haki za binadamu na uondoaji wa watu kwa nguvu.

Akiongea na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya zoezi la uhamishaji wananchi kwenye eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi amesema hakuna haki za binadamu zinazovunjwa, kwani zoezi linafanyika kwa faida ya wananchi.

“Serikali inatambua kwamba jumuiya na asasi mbalimbali za nje ya nchi zinaweza zikatoa maoni yao kwa kadri zinavyofahamu. Lakini ni muhimu wahusika wote wakatafuta ukweli” amesema Matinyi.

Kauli ya Matinyi inakuja siku chache baada ya Bunge la Ulaya kutoa azimio la kupinga mpango wa Serikali ya Tanzania kuwaondoa wananchi waliopo katika Hifadhi ya Ngorongoro.

Taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa za haki za binadamu zimekuwa zikilalamikia zoezi hilo kuwa linakiuka haki za binadamu kwa wakazi wa Ngorongoro ambao wengi wao ni jamii ya Wamasai.