The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Watu takribani 21 wameripotiwa kupoteza maisha baad aya kuangukiwa na ukifusi wakiwa katika shughuli za machimbo ya madini katika Mgodi wa Ng’alita, Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu.

Tukio hilo limetokea alfajiri ya  Januari 13 2024. Kamati ya ulinzi ya mkoa wa simiyu ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa simiyu Dkt Yahaya Esmail Nawanda wameshiriki katika zoezi la ukoaji ambapo kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo, miili 21 imetolewa nje ya mgodi huo huku mvua zinazoendelea kunyesha mkoani hapo zikizuia zoezi la uokoaji.

Chanzo cha kuanguka kwa kwa kifusi hicho inatajwa kuwa ni mvua zinazoendelea kunyesha katika mkoa huo. Akizungumza na waandishi wa habari, mkuu wa mkoa Dkt Yahaya Esmail Nawanda ameagiza kusimamishwa kwa shughuli za uchimbaji wa madini katika mgodi huo hadi hapo ambapo hali ya kiusalama itakapoimarika.

Akitoa salamu za pole kwa wafiwa, kupitia ukurasa wake wa X na kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii Rais Samia ameeleza kupokea kwa masikitiko taarifa  hiyo na kuahidi kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vikishirikiana na uongozi wa mkoa wa Simiyu vinaendelea na juhudi za kutafuta miili mingine ambayo bado imekwama ndani ya kifusi huku idadi kamili ya waliokuwa ndani ya mgodi huo ikiwa haijawekwa wazi bado.

Tukio hili linatokea ikiwa ni siku moja tu imepita tangu Mvua zinazoendelea zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali ya nchi  kusababisha madhara kuzuia shughuli za usafiri na shughuli mbalimbali za kijamii mkoani Mwanza huku mkoani Mbeya zikisomba na kuhamisha makaburi.

Mamlaka ya hali ya hewa nchini ilitoa taadhari na kutaja mikoa mabayo itaathirika na mvua hizi za elnino zitakazoendelea kunyesha hadi mwezi wa mpili hapa nchini. Simiyu ni miongoni mwa ameneo ambayo yalianishwa na mammlaka hiyo kukabiliwa na mvua za elnino.