The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, wameipitisha rasmi Somalia kuwa mwanachama mpya wa jumuiya hiyo inayokuwa na wanachama nane sasa.

Wakuu hao wa nchi wa jumuiya hiyo wamefikia uamuzi huu wakati wa mkutano wa kawaida wa 23 wa wakuu wa nchi uliofanyika jijini Arusha nchini Tanzania, Novemba 24, 2023.

Uamuzi huu wa wakuu wa nchi umefanyika kwa mujibu wa Ibara ya 23 ya Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Akizungumza mara baada ya uamuzi huo, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amesema wananchi wa Somalia wameheshimishwa kuwa sehemu ya jumuiya hii ya kikanda.

“Uamuzi huu umetupa matumaini mapya. Matumaini ya mustakabali wa fursa na ustawi kwa Somalia, kupitia ushirikiano huu wa kikanda” amesema Rais Mahamud.