The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Mwanyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Joyce Shebe, amewataka watumiaji wa vyombo vya habari hasa vya mtandaoni wahakikishe wanaheshimu utu na haki za binadamu pale wanapokuwa wanafuatilia habari mbalimbali ili kuepusha ukatili wa kijinsia mitandaoni.

Shebe ametoa wito huo leo Jumatano wakati alipokuwa akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama hicho yaliyifanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere.

Ukatili wa kijinsia wa mtandaoni ni tatizo kubwa linalowakumba wanawake wengi ulimwenguni kote.

Nchini Tanzania, ripoti zinaonesha kwamba ukatili wa kijinsia mitandaoni huwalazimisha wanawake wengi kuacha kutumia majukwaa hayo.

Hali ni mbaya zaidi kwa wanawake waliopo kwenye siasa ambao wanaripoti kukabiliwa na tatizo hilo kila mara watumiapo majukwaa hayo.