Mbeya. Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania(TEC) Mhashamu Baba Askofu Gervas Nyaisonga ametoa salamu za pole kwa wahanga waliokumbwa na maafa wilayani Hanang, mkoa wa Manyara kwa niaba ya Kanisa Katoliki Tanzania.
Ameyasema hayo leo disemba 6, 2023 ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameishukuru Serikali kwa jitihada ilizozifanya katika zoezi la uokoaji linaloendelea.
Pamoja na salamu hizo za pole TEC wamewasilisha msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula, dawa, mablanketi na mbegu za mazao.
Askofu Nyaisonga amewataka Watanzania wote kutoa ushirikiano kwa wahanga na kuendelea kuwaombea majeruhi katika kipindi hiki kigumu.