TIC imewataka wenye uwekezaji kama vile wa kiwanda, jengo, hospitali, shamba kubwa, biashara na kadhalika ambao wanatafuta mbia wawasilishe taarifa kamili za mradi husika ili waweze kutafutiwa washirika.
Kwa mujibu wa TIC, taarifa hizo zitawekwa kwenye kijarida cha kidijitali na kutumiwa kipindi kituo hiko kinanadi fursa za uwekezaji nchini katika mataifa mbalimbali duniani.
TIC ilianzishwa mwaka 1997 kwa lengo la kutangaza fursa za uwekezaji nchini katika sekta mbalimbali kwa wawekezaji wa ndani na nje, lakini pia kufanikisha uwekezaji kwa njia ya ubia kati ya wazawa na wawekezaji kutoka nje.