The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Watu 14 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na ajali ya basi lenye namba ya usajili T 336 DPW kampuni ya Baraka Classic lililokuwa linatokea Newala kwenda Dar es salaam majira ya asubuhi.

Chanzo cha ajali hiyo iliyotokea eneo la Mputa, halmashauri ya Mtama inadaiwa kuwa hitilafu ya breki iliyokuwepo katika gari hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, ACP John Makuri amesema kati ya watu 14 waliopoteza maisha, 12 walikuwa wasafiri na wawili walikuwa watemebea kwa miguu. Kwa upande wa majeruhi ni 26.

Hii ni ajali ya pili kutokea hivi karibuni hapa mkoani Lindi kwani Oktoba 6, 2023 watu saba waliripotiwa kufariki na wengine 22 kujeruhiwa kufuatia ajali ya basi aina ya Scania la Kampuni ya Saibaba, ambalo liligongana na basi dogo aina ya Tata katika kijiji cha Kiwawa, Wilaya ya Kilwa mkoani humo.