The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Samia Amrudisha Mkurugenzi wa Bima Aliyetumbuliwa na Magufuli

Sekta ya Bima ni sehemu muhimu ya uchumi wa Tanzania ambao mpaka Juni 2021, kampuni za bima zilikua na mali za Shilingi trilioni 1.2, huku bima zikiweka amana za takribani Shilingi bilioni 346 katika mabenki. 

subscribe to our newsletter!

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne, Januari 4, 2021, amemteua Baghayo Abdalah Saqware kama Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima (TIRA) ikiwa ni takriban miaka mitatu tangu Saqware ‘atumbuliwe’ na Rais wa awamu ya tano hayati John Magufuli.

Uteuzi wa Saqware, ambao ulianza Januari 1, ni moja kati ya teuzi zilizofanywa na Rais Samia na kutangazwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu Jaffar Haniu.

Wengine ni Charles Jackson Itembe aliyeteuliwa kama Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Eneo Maalum la Mauzo ya Nje (EPZA) na mwengine ni Ernest Maduhu Mchanga aliyeteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Pamoja ya Fedha.

Haijulikani kwa nini Rais Samia ameamua kumrejesha Saqware, ambaye kabla ya uteuzi wake wa mara ya kwanza hapo Februari 2017 alikuwa akifundisha katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), kwenye eneo la usimamizi wa shughuli za bima nchini.

Wakati Rais Magufuli anamteua Saqware Februari 2017 soko la bima lilikua ni takribani Shilingi bilioni 660 na likichangia asilimia 0.55 ya pato la taifa. Mpaka wakati anatumbuliwa, mnamo Juni 2019, soko la bima lilikua ni takribani Shilingi bilioni 800 huku kukiwa na kampuni za bima 32 zenye leseni.

Bima ni sehemu muhimu ya uchumi wa Tanzania ambao mpaka Juni 2021, kampuni za bima zilikua na mali za Shilingi trilioni 1.2, huku bima zikiweka amana za takribani Shilingi bilioni 346 katika mabenki.

Kutokana na umuhimu huu wa bima katika uchumi, Saqware anakabiliwa na mambo kadhaa kama bosi mpya wa TIRA ambayo wadau wa sekta ya bima wanadhani yanaweza kusaidia kuongeza mchango wa sekta ya bima kwenye ukuaji wa uchumi nchini.

Saqware anakabidhiwa TIRA wakati ambao kuna kusuasua kwa mwenendo wa baadhi ya makampuni ya bima.

Hali hii inadaiwa kutokana na uchanga wa sekta ya bima pamoja na ufinyu wa soko ambapo sehemu kubwa limejikita katika kile wataalam wanakiita general insurance, ambazo ni zile bima maarufu kama vile za vyombo vya moto, bima za majumbani, bima za kusafiri, na bima za afya.

Hali hii imepelekea kufungwa kwa kampuni kadhaa za bima, ikiwamo Star General Insurance, AAR Insurance, kitu kinachodaiwa kutokana na hali ngumu ya kibiashara.

Ni matumaini ya wadau wa sekta ya bima nchini kwamba Saqware atachukua hatua zitakazosaidia upanuzi wa wigo wa bima kutoka kwenye general insurance. Kufanikisha hili, bosi huyo atalazimika kuweka mazingira rafiki yatakayowezesha ushirikiano wa karibu kati ya ofisi yake na kampuni za bima katika kuongeza ufahamu wa wananchi juu ya bidhaa mbalimbali za bima.

Pia, kumekuwepo na malalamiko mengi ya kila wakati juu ya namna kampuni za bima zinavyozungusha wateja hata katika madai yaliyothibitishwa na yenye uhakika. Moja ya sababu kubwa ya makampuni ya bima kuzungusha wateja ni pale ambapo wanapokuwa hawana fedha za kutosha, mara nyingi ni sababu ya kuweka kiwango kikubwa katika uwekezaji  wa amana za serikali au katika mabenki.

Wadau wamekuwa wakipendekeza kwamba kuna umuhimu wa kuhakikisha makampuni ya bima yanaacha fedha za kutosha katika kulipa madai yanayowakabili.

Kuinuka kwa Bancassurance, ambapo ni hali ya mabenki kufanya kazi ya uwakala wa bima, ni fursa na tishio kwa kampuni za bima.

Bancassurance ni fursa hasa ambapo benki nyingi zina nafasi ya kupata wateja wengi kwa mkupuo kupitia bidhaa zao za mikopo na mtandao walionao. Tishio, kwa upande mwingine, linakuja pale benki zinapotumia nguvu ya soko kusukuma kampuni za bima kufanya kulingana na matwakwa yao na sio sera na kanuni za utendaji wa bima.

Ni katika muktadha huu ambapo wadau wamekuwa wakihizihimiza mamlaka zinazosimamia sekta ya bima nchini umuhimu wa kuyalinda makampuni ya bima ili yasijekupotea.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

One Response

  1. INSURANCE INDUSTRY? They take from the insured but are reluctant to pay out claims from the insured!! That means they are perfect leeches!!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts