The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Bei za Vyakula, Vinywaji Baridi Bado Mwiba kwa Watanzania

Kwa mujibu wa NBS, baadhi ya vyakula vilivyoripotiwa kupanda bei ni pamoja na mchele, mahindi, unga wa ngano, unga wa mahindi, mboga mboga, viazi vitamu, viazi mviringo, ndizi na maharage.

subscribe to our newsletter!

Dar es Salaam. Bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi nchini Tanzania zimeendelea kuongezeka na kufikia asilimia 6.3 kwa Januari 2022 kutoka mfumuko wa bei wa asilimia 4.9 uliosajiliwa Disemba 2021.

Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Februari 8, 2022, na Ofisi ya Taifa la Takwimu (NBS) kuhusu hali ya mfumuko wa bei za bidhaa kwa mwezi Januari 2022.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baadhi ya vyakula vilivyoripotiwa kupanda ni pamoja na mchele, mahindi, unga wa ngano, unga wa mahindi, mboga mboga, viazi vitamu, viazi mviringo, ndizi na maharage.

Pamoja na ongezeko hilo la mfumuko wa bei wa vyakula na vinywaji baridi, wastani wa mfumuko wa bei wa taifa kwa ujumla kwa Januari umepungua hadi asilimia 4.0 kutoka asilimia 4.2 ilivyokuwa kwa mwezi Disemba 2022. 

Kwa mujibu wa taarifa ya NBS, ongezeko la bei za vyakula na vinywaji baridi halikuweza kuathiri kwa kiasi kikubwa wastani wa mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Januari 2022, kutokana na kushuka kwa bei za bidhaa zisizo za chakula katika kapu la watumiaji.

Bidhaa hizo  zisizo za chakula zilizotajwa kushuka bei ni  pamoja na mavazi kutoka asilimia 4.5 hadi asilimia 2.8,viatu kutoka asilimia 4.6 hadi asilimia 4.4,kodi ya pango kutoka asilimia 4.4 hadi asilimia 1.2, magodoro kutoka asilimia 12.3 hadi asilimia 7.3, majokofu kutoka asilimia 4.2 hadi asilimia 1.5.

Bidhaa nyingine ni vyerehani kutoka asilimia 9.1 hadi asilimia 5.0, Simu janja kutoka asilimia 3.5 hadi asilimia 3.3, vyombo vya nyumbani kama sahani kutoka asilimia 16.7 hadi asilimia 3.6, rungina kutoka asilimia 3.5 hadi asilimia 1.2 na malazi kwenye hoteli na nyumba za kulala wageni kutoka asilimia  6.6% hadi asilimia 2.9.

Wataalam wa masuala ya kiuchumi waliieleza The Chanzo hivi karibuni kwamba kupanda kwa bei za bidhaa muhimu kama chakula inaweza kuwa ni matokeo ya ukame ambao umeyakumba baadhi ya maeneo nchini, pamoja na sababu nyengine kama vile janga la UVIKO-19.

Kupungua kwa wastani wa mfumuko wa bei wa taifa  kumeshuhudiwa pia katika nchi nyingine za Afrika mashariki ikiwemo Kenya na Uganda. 

Kwa upande wa Kenya, mfumuko wa bei umepungua kutoka asilimia 5.73 mwezi Disemba 2021 hadi kufikia asilimia 5.39. Huku Uganda mfumuko wa bei ukipungua kutoka asilimia 2.9 Disemba mwaka jana hadi kufikia asilimia.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts