The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Serikali Yatimba Kiwanda cha Pepsi Kufuatia Malalamiko ya Wafanyakazi

Ziara hiyo ambayo ilidumu kwa muda wa takriban masaa nane, ikijumuisha ukaguzi wa kiwanda na kuhoji baadhi ya wafanyakazi, inakuja wiki moja tangu The Chanzo ichapishe habari za kufukuzwa kazi kwa viongozi wa wafanyakazi kiwandani hapo, hatua walioihusisha na harakati zao za kupigania haki na maslahi ya wafanyakazi.

subscribe to our newsletter!

Dar es Salaam. Maafisa wa Serikali kutoka Ofisi ya Kamishna wa Kazi, Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Idara ya Uhamiaji wamefanya ziara maalum kwenye kiwanda cha SBC Tanzania kinachozalisha vinywaji baridi kama Pepsi kilichopo eneo la Vingunguti jijini hapa, The Chanzo imeelezwa.

Ziara hiyo ambayo ilidumu kwa muda wa takriban masaa nane, ikijumuisha ukaguzi wa kiwanda na kuhoji baadhi ya wafanyakazi, inakuja wiki moja tangu The Chanzo ichapishe habari za kufukuzwa kazi kwa viongozi wa wafanyakazi kiwandani hapo, hatua walioihusisha na harakati zao za kupigania haki na maslahi ya wafanyakazi.

Wakati wa mahojiano maalum na The Chanzo, Said Ibrahim Stawi, ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwandani (TUICO), tawi la SBC Tanzania kabla ya kufukuzwa kazi alianisha madhila wanayokumbana nayo wafanyakazi wa kiwanda hicho.

Madhila haya ni pamoja na madai ya kuafanyishwa kazi bila ya mikataba; watu kufanyishwa kazi kama vibarua kwa zaidi ya miaka 20; na tuhuma za rushwa ya ngono ambayo wahanga wakubwa ni wafanyakazi wanawake.

Mengine yanahusisha watu kufanyakazi miaka mingi bila ya kuwepo kwa nyongeza ya mishahara; pamoja madhila udhalilishaji mahala pa kazi kama vile kukaripiwa kwa makosa madogo madogo na hata ubaguzi wa rangi unaoelekezwa dhidi ya wazawa.

“Serikali imefanya ziara ya kushitukiza hapa [kiwandani],” kilisema chanzo chetu ambaye ni moja kati ya wafanyakazi waandamizi kiwandani hapo. “Mpaka muda huu [saa 1:30 jioni] wapo kwenye chumba cha mkutano.”

Chanzo chetu kilieleza kwamba maafisa hao kutoka serikalini walifika hapo majira ya saa sita za mchana na kuondoka majira ya saa mbili kasoro za jioni.

“Walitembelea pia maeneo mbalimbali ya kiwanda na kuwauliza wafanyakazi kuhusu masuala mbalimbali ya manyanyaso,” kilisema chanzo chetu ambacho kwa sababu za kiusalama amekataa jina lake kuandikwa mtandaoni. “Na nadhani kuna watu watawajibishwa. Hiyo ni safi.”

Mnamo Machi 27, 2022, Naibu Waziri mwenye dhamana na masuala ya kazi Patrobas Katambi alitoa tamko lililoeleza kufahamu kwake uwepo wa malalamiko yaliyoibuliwa na wafanyakazi na kuahidi kuyafanyia kazi.

“Nimewaagiza [wahusika] kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za kazi,” tamko hilo lilimnukuu Katambi akisema. “Ikiwa ni kufanya uchunguzi wa kina juu ya yanayolalamikiwa na pili kufanya ukaguzi tena kwa mapya yatakayojitokeza na kuchukua hatua.”

Katambi aliwasihi wafanyakazi wasisubiri shida zikithiri kwenye maeneo yao ya kazi ndipo waibuke kutoa malalamiko yao, akiwataka kutoa taarifa mapema kwa mamlaka husika kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts