The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Yetu Microfinance Yafilisika, Yawekwa Chini ya Uangalizi wa Benki Kuu

BoT imesema kwamba benki hiyo kuendelea kutoa huduma za kibenki kutahatarisha usalama wa amana za wateja wake.

subscribe to our newsletter!

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza kuiweka chini ya usimamizi wake Yetu Microfinace Bank PLC kufuatia upungufu mkubwa wa ukwasi na mtajii wa benki hiyo, hali inayokwenda kinyume na Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya 2006 na kanuni zake.

Kwenye taarifa yake iliyotolewa leo, Disemba 12, 2022, BoT imesema kwamba benki hiyo kuendelea kutoa huduma za kibenki kutahatarisha usalama wa amana za wateja wake.

BoT imeisimamisha Bodi ya Wakurugenzi na uongozi wa Yetu Microfinance na kuteua Meneja Msimamizi ambaye atasimamia shughuli za benki kwa kipindi ambacho itakuwa chini ya usimamizi wa Benki Kuu ya Tanzania.

Yetu Microfinance Bank PLC imekuwa ikifanya biashara ya benki, hususan na watu binafsi, vikundi na wafanyabiashara wadogo wa vijijini na mijini nchini Tanzania tangu ilipopatiwa rasmi leseni na BoT hapo Februari 20, 2017.

Kwenye taarifa yake hiyo ya Jumatatu, BoT imesema kwamba shughuli za kibenki za Yetu Microfiance Bank Plc zitasimama kwa siku 90 kuanzia Disemba 12, 2022, ili kutoa nafasi ya kwa BoT kufanya tathmini juu ya hatua za kuchukua kukabiliana suala husika.

Wamiliki wa Yetu Microfiance Bank Plc ni wanahisa, ambapo taasisi ya  Youth Self Employment Foundation (YOSEFO) ndiyo inatajwa kumiliki hisa nyingi huku asilimia 84 ya hisa zilizobaki zinamilikiwa na wawekezaji wadogo wa Tanzania kupitia soko la hisa la Dar es Salaam.

Taarifa ya fedha kwa umma zilizokaguliwa za Yetu Microfince Bank Plc kwa mwaka ulioishia Disemba 31, 2020, inaonesha ilikuwa na mali jumla ya Sh19,504,027,000, dhima ya Sh10,941,052,000 na jumla ya fedha za wanahisa Sh8,562,976,000.

BoT imewatoa hofu Watanzania kwa kusisitiza kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki na taasisi za fedha kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha nchini.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *