The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Wahitimu wa Mwaka 2015 Kuwa Kipaumbele Nafasi za Ajira Serikalini

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Angellah Kairuki ameeleza kuwa wahitimu waliomaliza shule mwaka 2015 watakuwa kipaumbele katika nafasi za ajira zilizotangazwa.

subscribe to our newsletter!

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Angellah Kairuki ameeleza kuwa wahitimu waliomaliza shule mwaka 2015 watakuwa kipaumbele katika nafasi za ajira zilizotangazwa.

Ajira hizi ni zile 21,200 zilizotangazwa Aprili 12, 2023, za kada za ualimu na afya. Ambapo ualimu ikiwa ni ajira 13,130 na kada za afya ikiwa ni ajira 8070.

“Mheshimiwa Spika kwenye hili tuwahakikishie waheshimiwa wabunge katika mchakato huu tulionao sasa kwanza tutaanza na ajira za 2015, waliomaliza shule 2015.” Alifafanua Waziri Kairuki.

“Na tunaangalia maeneo matatu tu vigezo vyetu vikubwa la kwanza mwaka wa kuhitimu, la pili kwa elimu ni masomo na kwenye hili labda niliweke wazi ni masomo ya aina gani inawezekana wengine hawayajui.”

“Ni masomo ya sayansi ukiangalia fizikia, Kemia na baiolojia, lugha ya kingereza lakini pia kingereza na fasihi na wale wataalamu wetu wa ufundi katika maabara zetu za sayansi.” Alieleza zaidi Kairuki.

Hivi karibuni kumekuwa na mjadala mkali Bungeni huku baadhi ya wabunge wakipendekeza ajira hizo zitolewe kimajimbo, hata hivyo Kairuki amewatoa hofu wabunge na kuwaambia mchakato utafuata haki.

“Na niwahakikishie waheshimiwa Wabunge na kwenye hili kwa kweli niwaondolee lawama zote waheshimiwa wabunge wala wananchi wenu wasiwahukumu kwamba labda hukumsaidia mtu au lolote.”Aliendelea kufafanua Waziri Kairuki, “tutahakikisha kwa nguvu zetu zote tunasimamia kuhakikisha kwamba zoezi hili linaenda kwa haki.”

“Na wako hata viongozi ambao wamenipigia simu na nimesema siangalii kiongozi siangalii nani ni nani, tunatenda haki. Kwa sababu tusipofanya hivyo ndugu zangu mtu asiye mjua mtu tutajenga taifa ambalo huko mbele tutapata shida sana.”

Mwisho wa kutuma maombi ya ajira hizo ni April 25,2023, na maelezo kamili ya ajira hizo yanapatikana katika tovuti ya TAMISEMI.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *