Waraka wa Baraza la Maaskofu Katoliki uliotolewa Agosti 18,2023, kupinga mkataba wa Bandari kati ya Tanzania na Dubai,umesomwa leo katika misa mbalimbali za Kanisa Katoliki nchi nzima.
Waraka huo uliopewa jina la Sauti ya Watu, Sauti ya Mungu umeitaka serikali kuwasikiliza wananchi kwa kusitisha utekelezaji wa Mkataba uendeshaji bandari za Tanzania ulioridhiwa na Bunge Juni 10,2023.
“Tukisukumwa na dhamiri iliyo na lengo la kulinda rasilimali, mshikamano, amani, uhuru, na umoja wa kitaifa; tunathubutu kusema kuwa baada ya miaka 63 ya uhuru wa nchi hii, wananchi hawajapenda kuiachia bandari ya Dar es Salaam apewe mwekezaji mmoja aiendeshe kwa vile Watanzania wenyewe wana uzoefu wa kuiendesha,” inasema sehemu ya tamko hilo lilosainiwa na Maaskofu 37
“Hivyo tukiwajibika kimaadili, tunaona ni jukumu la serikali kusikiliza wananchi wanaotaka mkataba huu ufutwe.”
Waraka huo umeendelea kuzua gumzo sehemu mbalimbali Tanzania, lakini hii si mara ya kwanza kwa Baraza la Maaskofu kutoa waraka juu ya masuala mbalimbali ya kijamii uliozua gumzo kubwa.
Mwaka 2021, waliweza kutoa waraka juu ya janga la UVIKO-19, wakati ambao serikali ilikuwa ikieleza kuwa hakuna janga la UVIKO nchini. Pia mwaka 2018, kupitia waraka wa Kwaresma walizungumzia hali ya kidemokrasia nchini wakieleza kuwa kuna uvunjifu wa Katiba na sheria kwa kufungia vyombo vya habari na kuzuia shughuli za kisiasa.
Kanisa Katoliki liliingia nchini miaka 155 iliyopita, likikadiriwa kuwa na waumini zaidi ya milioni 15.
10 responses
Kwangu
Tunakosa wapi pa kuanzia,tulitegemea serikali kama mama wa watanzania,lakini lengo lao linalenga tofauuti,tunashukuru kwa mara ya kwanza kanisa kuacha woga kuyaona haya na kukemea hili,tunasubiri na jeshi na polisi wasijifanye wao wanasubiri kukamata watun hata kama pia wao wnajua linawaumiza ila wanaogopa kuharibu kibarua,hii haiko hivyo, wasikubali kutumwa wakamate watu wanaokemea mabaya wakati wanajuwa sio sawa kisa kulinda viongozi na serikali,tambua watanzania wana shida,tugawane tunachokipata kwa usawa tushirikishane kila mtu kwa uwezo wake na elimu yake nchi isonge mbele,acheni uchoyo hakuna mtu ataondoka na shilingi hapa duniani,haisaidii kitu wote tutaoza, tutambue kuwa Mungu atahukumu kwa matendo yetu,hivyo linda nafasi yako huko kwa Mungu
Kwakweli kama serikali haitazingatia waraka huu ambao kabla yake nyuma kuna maono,ushauri,wasiwasi na maonyo juu ya Taifa na wana Taifa kiusu mkataba wa bandari inakotupeleka ni pabaya sana na nchi hii inaweza kuwana hali mbaya kuliko hata Kongo ya Sasa.
Napingana na Baraza la maaskofu
Unapingana kwa fact zipi ? Maaskofu wameweka facts waraka umekuja baada serikali kiweka mabunzi masikioni
Tatizo la sisi wanadamu tunashindwa na hatutaki kuisikia sauti ya Mungu,lkn tungekuwa tayar kumpokea Yesu kuwa n mwokoz wa maisha Haya yote yasingetokea maana huu n ubinafsi
Huu ndiyo WAKATI wa kanisa kusimamia kama Ester la sivyo Mungu ataleta msaada mwingine Kwa wa Tz. Bigger up! Lakini pia Wana siasa Kwa IMANI zetu hebu tumwogopeni Mungu tufuateni viapo vyetu na uzalendo tulioridhishwa na watangulizi wetu. Mali zote tutaziacha.
hawa ndio hawipendi amani! mbona walishampelekea rais maoni yao wote kwa pamoja viongozi wa dini zote? hawa wana lao jambo, wamezoeshwa kudekezwa na kupewa hela za mkataba wa hovyo wa mwaka 1992 na pia wamezoea kupitisha mizigo hewa bandarini
Mi kinachonishangaza mpaka sa hivi sijaelewa ni kitu kimoja Kuna watu wanasema bandari inafaa wengine wanasema haifai kwani kigezi kinatumika kuukata na kuukubali
Hawa maaskofu ndio watakao leta vita Tanzania. Waraka wenyewe umejaa unafiki na udini