The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

‘Bangi Kama Tiba’:Serikali Yataka Umakini na Tafiti Juu ya Kuruhusu Matumizi ya Bangi

Serikali imesema jambo la kutoa kibali cha kuruhusu kilimo na matumizi ya bangi ni suala ambalo halitakiwi kufanyiwa maamuzi ya haraka, inabidi serikali ijipe muda kufanya tafiti za kutosha ili ifanye maamuzi yenye tija.

subscribe to our newsletter!

Serikali imesema jambo la kutoa kibali cha kuruhusu kilimo na matumizi ya bangi ni suala ambalo halitakiwi kufanyiwa maamuzi ya haraka, inabidi serikali ijipe muda kufanya tafiti za kutosha ili ifanye maamuzi yenye tija.

Haya yameelezwa leo April 15,2024, Bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Nkenge, Florent Laurent Kyombo aliyeuliza msimamo wa serikali baada ya baadhi ya nchi kuruhusu matumizi ya bangi kama tiba.

“Tunachokifikiri sisi ni kuanza kuwasiliana na vyuo vyetu kuanza kufanya hizo tafiti lakini mjadala wa kuikubali nchi iingie katika kibali cha kutumia bangi na utafiti wa namna moja au nyingine ni lazima tuwe na makubaliano ya pamoja,”alieleza Mhagama.

“Ni lazima kama nchi tufanye kwanza tafiti ili tuweze kufanya maamuzi hayo. Waheshimiwa Wabunge bangi mpaka sasa kama taifa tunaiona ni dawa ambayo ina madhara makubwa sana,inaharibu sana afya za vijana wetu.”

Mhagama ameeleza suala la bangi kuruhusiwa katika matumizi ya tiba lilifanyika ulimwenguni kupitia Kamisheni kuzuia madawa ya kulevya ambapo nchi nyingi wanachama zilipiga kura na kukubali jambo hilo.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts