The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Benki Kuu ya Tanzania Yapiga Marufuku Wakopeshaji Mitandaoni Kutuma Jumbe Za Madai Kwa Wasiohusika, Kudhalilisha Wadaiwa Mitandaoni

Muongozo wa Benki Kuu unazuia wakopeshaji wa kidigitali kudhalilisha wadaiwa wao mtandaoni na pia unalinda taarifa za mkopeshaji

subscribe to our newsletter!

Benki Kuu ya Tanzania imetoa muongozo kwa wakopeshaji wa kidigitali ambapo pamoja na mambo mengine muongozo huo umepiga marufuku wakopeshaji mtandaoni kutumia lugha za kudhalilisha, kuchapisha taarifa za waliokopeshwa mtandaoni au kutuma jumbe kwenye namba zilizopo katika simu ya aliyekopeshwa.

Muongozo huo uliosainiwa Agosti 2024, unakuja katika kipindi ambapo kumekuwa na ongezeko kubwa la taasisi mbalimbali zinazotengeneza App za kukopesha. Kampuni hizi zimekuwa  zikitupiwa lawama juu ya utendaji wao usiofaa. Mfano Juni 04,2024, baadhi ya Wabunge walilamika juu ya kuungwa kwenye makundi ya WhatsApp ambapo vitambulisho vya watu wanaosemwa kuwa na madeni vimekuwa vikitumwa.

“Wanafedheshesha watu. Wanarusha vitambulisho vya watu kwenye makundi, kwa hiyo watu wanadhalilishwa,” alieleza Mbunge  Jang’ombe Ali Hassan King.

Muongozo huo wa Benki Kuu unataka mkopeshaji kidigitali  kwanza kusajiliwa na Benki Kuu na pia mfumo wa kidigiti anaoutumia lazima uwe salama katika utumiaji.  Baadhi ya mambo ambayo muongozo umeyakataza ni pamoja na:

1. Kutumia vitisho, vurugu au njia zingine za kumuumiza aliyekopeshwa katika marejesho

2. Kutumia lugha za matusi kwa mteja au wadhamini wa mteja au namba zingine kwenye simu yake kwa nia ya kumdhalilisha

3. Kuangalia katika simu ya mteja namba zingine za simu kwa ajili ya kuwatumia meseji mteja anaposhindwa kulipa katika muda au asipolipa.

4. Kutuma taarifa binafsi za mteja katika mitandao kwa ajili ya kumdhalilisha

5. Kupiga simu au kutuma meseji kwa namba zingine zilizopo kwenye simu ya mteja

6.Mtoa mikopo hataruhusiwa kutumia mifumo ya ukopeshaji kuangalia namba za simu katika simu ya mteja, kuangalia simu alizopiga au kupokea. Pia hataruhusiwa kuangalia: meseji, picha, mitandao yake ya kijamii, email, mafaili au Applikesheni mbalimbali kama njia ya kumtambua mteja au kuendelea kuwa na mahusiano naye kama mkopeshaji

7. Mkopeshaji hataruhusiwa kuzitoa taarifa binafsi zilizokusanywa na kuchakatwa Tanzania kwa watu au taasisi zilizoko nje ya Tanzania, labda kwa ajili ya matengenezo na maboresho ya jukwaa la kukopesha.

8. Wakopeshaji mtandaoni hawaruhusiwi kuendesha jukwaa la kukopesha kabla ya kupata idhini ya Benki Kuu, lakini pia wakitaka kufunga hawatatakiwa kufunga majukwaa haya bila kupata idhini ya Benki Kuu.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *