The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Vitu Tisa vya Kushangaza Kuhusu Watoto Ambavyo Hukuvijua

Wazazi tunapotambua vitu hivi vidogo tunapata nafasi ya kuangalia malezi na maisha ya watoto wetu kwa mtazamo mpya.

subscribe to our newsletter!

Je, unajua kuwa watoto hucheka mara tano zaidi kuliko watu wazima kwa siku? Au kwamba mtoto wako anaweza kutambua maneno mengi sana kabla hajaanza kuzungumza? 

Mara nyingi wazazi huwa tunaangalia ukuaji wa mtoto kwa macho ya kawaida – kula, kulala, afya, kucheza na kusoma. Lakini ndani ya maisha ya kila siku ya mtoto, kuna mambo ya ajabu na ya kuvutia ambayo wanasayansi wamegundua. 

Ukweli huu mdogo unaweza kutusaidia kuelewa zaidi ulimwengu wa watoto, na pia kutupa mbinu mpya za kuwalea kwa upendo na maarifa.

Vitu hivyo ni pamoja na kwanza, ukweli kwamba watoto wachanga hutambua sauti ya mama mara tu wanapozaliwa. Tafiti zinaonesha kuwa ndani ya masaa machache baada ya kuzaliwa, mtoto mchanga anaweza kutofautisha sauti ya mama yake na sauti nyingine. Hii hujenga msingi wa uhusiano wa karibu na wa kipekee kati ya mama na mtoto.

Pili, watoto wadogo huelewa zaidi ya maneno wanayoweza kuzungumza. Kabla ya kuanza kuongea kwa ufasaha, watoto wa umri wa miaka miwili tayari wanaweza kutambua zaidi ya maneno 200, hata kama wanaweza kusema maneno machache tu. Hii ni ishara kuwa ufahamu wao huendelea mbele ya uwezo wao wa kuzungumza.

SOMA ZAIDI: Leo Tujadili Umuhimu wa Kuwasiaidia Watoto Kuelezea Hisia Zao 

Tatu, watoto hucheka takribani mara 300 kwa siku. Watu wazima wanacheka takribani mara 60 pekee kwa siku, lakini watoto hufika mara 300! Hili ni jambo la kufurahisha, kwa sababu ickheko kinaongeza furaha, huimarisha kumbukumbu, na hata huongeza kinga ya mwili.

Nne, ubongo wa mtoto hukua kwa kasi kubwa kabla ya miaka mitano kuliko wakati wowote wa maisha yake. Kufikia umri wa miaka mitano, ubongo wa mtoto tayari huwa umekua kwa asilimia 90 ya ukubwa wa ubongo wa mtu mzima. Ndiyo maana miaka hii ya awali ni muhimu sana katika malezi na makuzi ya mtoto, kujifunza, na kufunza tabia zilizo njema.

Tano, kujifunza lugha zaidi ya moja ni rahisi zaidi. Ni rahisi mtoto kujifunza lugha zaidi ya moja akiwa chini ya miaka saba. Watoto wanaojifunza lugha mbili kabla ya umri huou huwa na uwezo mkubwa zaidi wa kufikiri kwa ubunifu na kubadilika. Ubongo wao huwa na uwezo mkubwa wa kujifunza lugha katika miaka hii ya awali.

Sita, watoto huona rangi nyingi zaidi ya watu wazima. Macho ya watoto yanaweza kutambua vivuli vidogo vya rangi ambavyo watu wazima mara nyingi hukosa. Ndiyo maana mara nyingi watoto huona dunia kwa rangi zenye kuvutia na mwanga zaidi

Saba, mchezo kwa mtoto ni mazoezi ya ubongo. Wakati watoto wanacheza, iwe ni kucheza kmpira, kuruka kamba, au michezo ya kubuni, huwa wanaunda ujuzi wa kutatua matatizo, kuimarisha ubunifu na kujifunza kudhibiti hisia. Mchezo si burudani tu, ni msingi wa ujifunzaji kwa Watoto.

SOMA ZAIDI: Kwa Nini Watoto Wadogo Huwa na Hofu ya Watu, Hata Watoto Wenzao?

Nane, watoto wana hisia kali za harufu. Watoto mara nyingi hugundua harufu ambazo watu wazima hupuuza. Harufu ya maua, chakula au hata mvua huwa na uzito mkubwa zaidi katika kumbukumbu zao za utotoni.

Tisa, watoto hujifunza vyema kupitia nyimbo na hadithi. Maneno na midundo kutoka kwenye nyimbo na hadithi huwasaidia watoto kuhifadhi taarifa kwa muda mrefu zaidi. Ndiyo maana nyimbo za chekechea na simulizi za usiku hubaki moyoni ni zana za elimu na urithi wa utamaduni.

Kila siku katika maisha ya mtoto ni safari ya ugunduzi. Wazazi tunapotambua vitu hivi vidogo tunapata nafasi ya kuangalia malezi na maisha ya watoto wetu kwa mtazamo mpya. 

Hivyo basi mara nyingine mtoto akituuliza swali lisilo na mwisho au akacheka bila sababu, tukumbuke kuwa ubongo wake unakua, moyo wake unajifunza, na sisi tupo katikati ya safari hiyo ya ajabu.
Makala hizi za malezi huandaliwa na C-Sema, shirika lisilo la kiserikali linalojikita katika kuendeleza na kulinda haki za watoto Tanzania. Kwa maoni na ushauri, wapigie kwenye simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile, unaweza kuwapata kupitia kurasa za Facebook: Sema Tanzania, X: @SemaTanzania, na kupitia tovuti yao www.sematanzania.org.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×