Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kimewaomba wananchi kutoa taarifa ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yaliyofanyika nchini kuanzia Oktoba 28, 2025 hadi sasa.
Katika taarifa hiyo iliyochapishwa kwenye kurasa rasmi za rasmi TLS, imeeleza kwamba wananchi watume taarifa hizo kupitia WhatsApp na namba za simu +2557778157557 au baruapepe president@tls.or.tz.
“Kama kuna mwananchi yeyote ana taarifa za ukiukwaji wa sheria na uvunjifu wowote wa haki za binadamu kuanzia tarehe 28 Oktoba 2025 mpaka sasa anaombwa atume taarifa hiyo,” imeeleza taarifa ya TLS.
Katika taarifa hiyo, TLS imewaomba mawakili wote nchini kutoa msaada wa kisheria kwa haraka kwa wananchi wenye uhitaji.
Taarifa hii ya TLS inakuja ikiwa vitendo mbalimbali vya uvunjivu wa haki za binadamu na sheria vimeripotiwa kufanyika kabla na baada ya siku ya kupiga kura Oktoba 29, 2025 kupelekea vifo vilivyoripotiwa maeneo mbalimbali.