The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo Auawa kwa Risasi

CCM imetoa wito kwa wanachama wake kuwa watulivu wakati vyombo vya dola vikiendelea na uchunguzi wa kina

subscribe to our newsletter!

Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo, Mkoa wa Iringa, Bi Christina Nimrod Nindi, ameripotiwa kufariki katika Hospitali wa Tosamaganga alipofikishwa baada ya kushambuliwa kwa risasi na kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana siku ya jana akiwa nyumbani kwake.

Tukio hilo la kikatili limeripotiwa kutokea katika kitongoji cha Banawanu, kijiji cha Ugwachanya alipokuwa akiishi marehemu, ambapo uchunguzi wa awali wa Polisi umebainisha kuwa vijana watatu walivamia nyumbani kwake na kumshambulia.

Watekelezaji wa tukio hawakuchukua kitu chochote katika nyumba ya marehemu, zaidi wamemjeruhi binti wa marehemu maeneo ya usoni pamoja na jirani aliyejaribu kwenda kutoa msaada baada ya kusikia kelele.

CCM imeeleza masikitiko yake kufuatia tukio hilo na kutoa pole kwa familia, ndugu, viongozi, na wanachama wa CCM Mkoa wa Iringa kufuatia kifo hicho cha ghafla na cha kikatili.

Katika taarifa kwa umma iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, CCM imelaani tukio hilo na kuelezaa kuwa marehemu ameuawa wakati akiajiandaa kuhudhuria semina elekezi kwa makatibu wa chama hicho jijini Dodoma, Novemba 14, 2024.

Aidha CCM imetoa wito kwa wanachama wake kuwa watulivu wakati vyombo vya dola vikiendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria.

Haya yanajiri ikiwa zimepita siku tatu tangu kada mwingine wa chama chama hicho, Huruma Ally ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Itumba wilayani Ileje, Mkoa wa Songwe, kuvamiwa na watu wasiojulikana na kuvunjwa miguu yote miwili siku ya Jumamosi, Novemba 9, 2024, huku chanzo kikiwa bado hakijafahamika.

Jeshi la Polisi limeeleza kuendelea na uchunguzi na kutoa wito kwa mtu yeyote mwenye taarifa zinazoweza kusaidia kupatikana kwa wahalafu hao atoe ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts