The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Bolt Yatangaza Utekelezaji wa Viwango Vipya vya Nauli Kuanzia Ijumaa, Mei Mosi

Watoa huduma katika sekta ya usafiri wa mtandao nchini kampuni ya Bolt Tanzania imetangaza kuanza utekelezaji wa ongezeko la nauli kwa asilimia 22 kuanzia Ijumaa, Mei 1, 2026.

subscribe to our newsletter!

Watoa huduma katika sekta ya usafiri wa mtandao  nchini kampuni ya Bolt Tanzania imetangaza kuanza utekelezaji wa ongezeko la nauli kwa asilimia 22 kuanzia Ijumaa, Mei 1, 2026.

Hatua hii inakuja baada ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kutangaza viwango vipya vya nauli kwa mabasi ya masafa marefu, mabasi ya mijini (daladala), teksi mtandao na pikipiki mtandao kufuatia kupanda kwa bei za mafuta kwa takribani asilimia 33.4.

Bolt Tanzania kupitia taarifa yake kwa umma imeeleza kuwa marekebisho hayo ya viwango vya nauli ni sehemu ya utekelezaji wa hatua za udhibiti zilizolenga kuimarisha uthabiti wa sekta ya usafiri kipindi ambacho gharama za uendeshaji zimepanda. 

“Mafuta yanaendelea kuwa miongoni mwa gharama kubwa kwa madereva, na muundo mpya wa nauli unakusudia kupunguza athari za shinikizo endelevu la bei za mafuta,” imeeleza taarifa ya Bolt.

Kupitia Gazeti la Serikali toleo Na. 16 la Aprili 17, 2025, tangazo la LATRA la marekebisho ya viwango vya nauli kwa huduma za teksi mtandao zenye uwezo wa kubeba abiria wasiozidi wanne safari isiyozidi kilomita moja nauli kiwango cha chini ni shilingi 4,000 na kiwango cha juu 5,000.

Huku nauli ya kuanzia safari (kwa tripu) kwa aina hiyo ya usafiri kiwango cha chini ni shilingi 1,100 na kiwango cha juu ni shilingi 1,200. Nauli kwa kilomita kiwango cha chini ni shilingi 1,100 na shilingi 1,300, nauli kwa dakika kiwango cha chini ni shilingi 120 na kiwango cha juu ni shilingi 150.

Pikipiki mtandao za magurudumu mawili na kubeba abiria mmoja au kama zinavyofahamika bodaboda, safari isiyozidi kilomita moja kiwango cha chini ni shilingi 1,500 na kiwango cha juu ni shilingi 2,000. Nauli ya kuanza safari kwa tripu ni kati ya shilingi 400 mpaka 500, Nauli kwa kilomita nayo ni shilingi 400 mpaka 500, na kwa upande wa nauli kwa dakika ni shilingi 90 mpaka 110.

Kwa upande wa Bajaji au Pikipiki mtandao za magurudumu matatu na kubeba abiria wasiozidi watatu, safari isiyozidi kilomita moja (1) ni shilingi 3,000 mpaka shilingi 4,000. Nauli ya kuanzia safari (kwa tripu) ni shilingi 500 mpaka 700, nauli kwa kilomita ni 700 mpaka 900, nauli kwa dakika ni shilingi 90 mpaka shilingi 110.

Viwango hivyo vipya vilivyotangazwa vinajumuisha pia ada ya kuita usafiri kwa tripu ambapo kiwango kwa asilimia inatofautiana kulingana na aina ya usafiri. Pia kamisheni ni kati ya asilimia 10 mpaka 20 kwa aina zote za usafiri, huku tozo ya Latra ni asilimia 0.5 kwa nauli kiwango cha chini na asilimia 1 kwa nauli ya kiwango cha juu.

Katika taarifa  yake Bolt Tanzania imeeleza kuendelea kushirikiana kwa karibu na mamlaka ili kuimarisha mfumo thabiti na unaozingatia kanuni katika sekta ya usafiri wa mtandao wakati wa kipindi hiki cha mpito.

“Bolt inabaki na dhamira ya uwazi, usalama na uendelevu wa muda mrefu katika mfumo wa usafiri nchini Tanzania.”

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×