The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Polisi Yathibitisha Kumshikilia Damour Aliyeripotiwa Kuchukuliwa na Watu Saba Nyumbani Kwao Mburahati

Katika taarifa ya Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Polisi wameeleza kuwa walimkamata Damour siku ya Jumamosi, Mei 2, 2026 majira ya saa tatu asubuhi maeneo ya Mburahati kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uhalifu.

subscribe to our newsletter!

Jeshi la Polisi Tanzania limetoa taarifa kwa umma kuwa linamshikilia Damour Massoumbe Nyakairo kwenye kituo cha Polisi Chang’ombe, saa 36 baada ya taarifa za kuchukuliwa na watu saba nyumbani kwao Mburahati kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Katika taarifa ya Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Polisi wameeleza kuwa walimkamata Damour siku ya Jumamosi, Mei 2, 2026 majira ya saa tatu asubuhi maeneo ya Mburahati kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uhalifu.

Taarifa hiyo ya Polisi imeeleza kuwa hatua za kiupelelezi zinakamilishwa ili aweze kufikishwa kwenye vyombo vingine vya kisheria.

Kufuatia kusambaa kwa taarifa za Damour kuchukuliwa na watu saba nyumbani kwao Mburahati siku ya Jumamosi, The Chanzo ilimtafuta Lilian Swai ambaye ni mama wa Damour majira ya saa nane mchana ambaye alithibitisha kushuhudia mtoto wake akichukuliwa na watu saba ambao hawakuweza kujitambulisha wala kueleza wapi wanampeleka.

“Wameondoka naye hatujui kapelekwa wapi. Wametoka huko watu saba wakaja, mimi nashangaa watu wanakimbia mvua au wanakimbia nini? Moja kwa moja wanamfuata Damour na mimi nimekuwa hapa. Wakamshika, wawili wanamshika na mmoja akatoa pingu mfukoni akamfunga. Nikauliza kuna nini [wakasema] ‘tutajua huko huko’, nyie nani? Wakasema ‘tutajuana huko huko’,” alieleza Lilian Swai.

Taarifa ya Polisi imeeleza kuwa Damour ametoa ushirikiano wa maelezo kwa Polisi.

“Baadhi ya ndugu zake tangu alipokamatwa walijulishwa na kwenye mahojiano ya awali ametoa ushirikiano wa kueleza mambo mbalimbali,” imeeleza taarifa ya Polisi.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×