Ukiachilia ufugaji ambao ndiyo umekuwa nguzo kubwa na kitega uchumi kwa Wamaasai na wenyeji wa Ngorongoro walio wengi, kabla ya mwaka 2009 Wamaasai walikuwa pia wakijihusisha na kilimo cha kujikimu. Mwaka 2009, hata hivyo, Serikali Rais Jakaya Mrisho Kikwete iliondoa kilimo cha kujikimu katika Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCA), jambo ambalo limepelekea kushamiri kwa janga la njaa katika eneo hilo. Serikali, kwa kutokujali wenyeji wa eneo, ilishindwa kuweka njia mbadala na thabiti ambazo zingewawezesha...