The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Kaya 120 zakosa makazi kutokana na mafuriko wilani Kilosa, Morogoro

Kaya takribani 120 katika vijiji vitatu vya kata ya Nyameni Zombo wilayani Kilosa mkoa Morogoro hazina makazi kutokana na athari za mafuriko yaliyosababishwa na mto  Miombo kujaa maji hapo jana. 

Mafuriko hayo yamepelekea uharibifu wa makazi, miundombinu ya barabara na madaraja hali ambayo imepelekea Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka na timu yake  kutembea zaidi ya umbali wa kilomita 5 ndani ya maji ili kujinusuru baada kuzingirwa na maji wakati akikagua zoezi la uokoaji wa wananchi.

Hapo jana, Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) ilitoa angalizo juu ya uwepo wa hali mbaya ya hewa inayoambatana na  mvua kubwa zinazotarijiwa kunyesha siku tatu mfululizo hadi tarehe 21 Machi, kwenye mikoa ya Pwani ya bahari ya Hindi. 

TBS yasema msaada wa chakula kutoka Marekani ni salama

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesema msaada wa chakula ikiwemo mchele ulioongezwa virutubishi na maharage  uliotolewa na Wizara ya Kilimo ya Marekani kwa ushirikiano na Taasisi ya Jumuiya za Kimataifa katika baadhi ya Shule za Mkoa wa Dodoma ulifuata taratibu za uingizwaji wa chakula nchini.

Taarifa ya TBS iiliyotolewa inaeleza kuwa chakula hiko kilifanyiwa ukaguzi na uchunguzi wa kimaabara na kuthibitishwa kuwa ni salama kwa matumizi. 

kuingizwa kwa msaada huo kumeibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya watu  wameonyesha mashaka juu ya usalama wa chakula hicho.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ni miongoni mwa watu waliohoji suala hilo na kudai kuwa waingizaji hawakupaswa kuagiza chakula hicho kutoka nje ya nchi kwa kuwa Tanzania ina hazina kubwa ya mchele na kuongeza kuwa kama ni virutubishi vingeongezwa kwenye mchele wa hapa nchini.