The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limezindua kampeni kwa wanafunzi wa shule ya “Tuwaambie kabla hawajaharibikiwa” kwa lengo la kupinga ukatili wa kijinsia na unyanyasaji kwa wanafunzi wawapo masomoni.

Kampeni hiyo imezinduliwa na Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Benjamin Kuzaga, Agosti 28, 2024 ambapo alizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mbeya Day  kutorubuniwa na kutokufumbia macho vitendo vya ukatili ambavyo vinakatisha ndoto zao.

Hata hivyo amewataka wanafunzi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kitengo cha dawati la jinsia, walimu, wazazi, walezi na hata viongozi wa dini pindi wanapoona viashiria vya matukio ya ukatili.

Kampeni hii inajili baada ya matukio ya ukatili kwa wanafunzi kuongezeka, itakumbukwa kuwa Agosti 23, 2024 mwalimu mmoja wilayani Kyela alihukumiwa kifungo miaka 30 kwa kosa la kumnajisi mwanafunzi wake,13.