Hali ya mitaa ya Kariakoo kwa siku ya leo Juni 24,2024, ni ya ukimya baada ya maduka katika eneo hilo muhimu la biashara kufungwa.
Maduka katika mitaa maarufu ya biashara na misongamano kama mtaa wa Congo, Msimbazi, Uhuru yote yalikuwa yamefungwa.
Katika baadhi ya maeneo matangazo yameonekana yenye kichwa, Kufunga Biashara Zetu, “Tangazo kuanzia leo 24/6/2024 tunafunga maduka yetu kwa muda usiojulikana mpaka Bunge litakapo ondoa sheria kandamizi zinazopora mitaji ya wafanyabiashara,” ilisoma sehemu ya tangazo hilo.
Vipeperushi juu ya mgomo huu vilianza kusambaa wiki iliyopita, huku viongozi wa wafanyabiashara hao wakionesha kuwa havikutoka kwao.
Polisi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wametoa onyo kwa wafanyabiashara hao.