The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Mtandao wa Wadau Wanaopinga Rushwa ya Ngono ambao una wanachama zaidi ya 300 umekipinga vikali kipengele cha 10(b) kilichopo kwenye Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wa mwaka 2024 kinachoeleza kwamba mtu ambaye atabainika kudai au kushwawishi kutoa rushwa ya ngono basi naye atashtakiwa.

Kipengele hicho kimeenda mbali zaidi na kueleza kuwa endapo mtu huyo atakutwa na hatia basi atahukumiwa kulipa faini au kufungwa jela na pengine kukumbana na adhabu zote kwa pamoja.

Hivyo, wadau hao wanaona kwamba kipengele hicho kitakwenda kurudisha nyuma jitihada zao za muda mrefu za kuhakikisha watu wanaoombwa rushwa ya ngono wanajitokeza hadharani, kwani watakuwa waoga kwa sababu wanaweza kushtakiwa kwa kudaiwa kuwa walidai au walishawishi kutoa rushwa ya ngono.

Wakizungumza na The Chango wadau hao wamefunguka mambo mbalimbali ambayo unaweza kuyasikiliza pamoja na mipango yao ya kwenda bungeni kutoa maoni yao ya kupinga kipengele hicho.

Ingia https://youtu.be/WmHUbjTP4W0?si=tZENDbn_E0xeJmTI