The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Zanzibar. Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Abdul-Gulam Hussein amesema Serikali itaziungunisha shule 217 kwenye mkonga wa taifa ili kuwawezesha wanafunzi wa skuli hizo kusoma kiuhalisia masuala ya kidijitali.

Hussein amesema hayo kwenye Baraza la Wawakilishi wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Mwanakwerekwe, Ameir Ali Ameir aliyetaka kufahamu kama juhudi za kuanzisha masomo ya kidijitali zinaenda sambasamba na uwepo wa huduma ya mtandao.

“Wizara tunakwenda kuziunganisha skuli 217 katika mkonga wa taifa, skuli hizi ziko maeneo mbalimbali za vijiji na mjini. Tukifanya hivyo tutakwenda sasa kuimarisha utoaji wa elimu ya kidigitali.” Amesema Abdul-Gulam.

Hadi kufikia 2023 Zanzibar imeanzisha madarasa maalum ya kidijitali yaani ‘smart class’ katika shule ya sekondari Mtakuja iliyopo Mjini Magharibi, na lengo ni kutanua aina hiyo ya madarasa visiwani Unguja na Pemba.

Imeandaliwa na Najjat Omar