Serikali imetoa tahadhari juu ya madhara yanayoweza kutokea kwenye uchumi sababu ya vita inayoendelea Ukraine lakini ni maeneo yapi hasa tunaweza kuguswa?
- Kuongezeka kwa bei ya unga wa ngano
Katika soko la dunia tayari bei ya ngano imeongezeka. Hali hii lazima itaonekana nchini kwani takribani 90% tunategemea ngano kutoka nje ya nchi, huku ngano nyingi ikitokea Urusi nchi ambayo kwa sasa haiwezi kufanya biashara sababu ya vikwazo
Ngano ina mnyororo mrefu hasa katika biashara ndogondogo. Suluhu ya kudumu ya tatizo hili ni kuamua kutumia uwezo uliopo kuzalisha ngano, kwani uwezo upo ingawa hakuna mipango ya moja kwa moja juu ya zao hili. Hii itasaidia pia kupunguza matumizi makubwa ya fedha za kigeni katika kununua ngano
- Kuongezeka kwa bei ya mafuta
Kwa mwaka 2020 tulitumia takribani trilioni 2.9 kununua mafuta na mwaka 2021 tulitumia takribani trilioni 4.9 kununua mafuta, kila bei inavyoongezeka lazima tutumie zaidi. Urusi ni mmoja wa wauzaji wakubwa wa mafuta duniani, hali tete juu ya uwezo wake kuuza mafuta inatosha kupandisha bei ya mafuta
Kwenye mafuta hakuna namna ya kukwepa ingawa tunaweza kupunguza maumivu kwa kuongeza mauzo ya vitu vyetu vya thamani. Jinsi unavyouza zaidi vitu vya thamani kama dhahabu ndivyo shilingi inavyoimarika hivyo kufanya hata gharama za kununua nje kutokupitiliza.
Hata wakati huu, dhahabu imeongezeka bei kwa kiasi kikubwa. Kuna madini mengine yanayoelekea kuwa na thamani kubwa kama dhahabu ikiwemo chuma, Nickel, cobalt na graphite haya yote tunayo nchini ingawa uanzaji wa miradi hii imekua ikisua sua
Ni vyema serikali ikaharakisha baadhi ya miradi hii ya madini haya. Sehemu ndogo inayotokana na mauzo ya madini haya yanaweza kutengeneza mfuko wa kukabiliana na kichefuchefu cha bei ya mafuta (fuel stabilization fund)
- Bidhaa zingine za majumbani
Kwa mwaka 2020 tulitumia trilioni 5.6 kununua bidhaa za majumbani na kwa mwaka 2021 tumetumia trilioni 6.8. Hii ni fedha kubwa kunahitajika jitihada za kupunguza hasa kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa nchini, mfano mafuta ya kula.
Mahitaji ya mafuta ya kula nchini ni tani 570,000 lakini uzalishaji ni tani 205,000 tu. Tani 365,000 tunaagiza nje ya nchi, mafuta ni moja ya bidhaa inayotegemewa kupanda. Kwani Urusi ni mmoja wa wazalisha wakubwa pia wa malighafi za mafuta.
Inategemewa nchi nyingi za magharibi nazo zitaangalia Asia na Afrika katika kutafta mafuta, ikimaanisha bei lazima ipande. Tanzania ina kila kitu kuwezesha kujitegemea kwenye mafuta ya kula, kuanzia nazi, mawese, pamba, ufuta, alizeti na ardhi yenye rutuba. Hatujamua kikamilifu kujitegemea kwenye hili
- Mdororo katika sekta ya utalii
Wakati Corona inaingia jitihada zilifanyika kufungua masoko mapya ya utalii. Masoko hayo mapya yalikua ni Urusi, Ukraine na Poland. Kwa mwaka 2020, Urusi iliongoza kwa kuleta watalii wengi zaidi Tanzania na kwa mwaka 2021 ni nchi ya pili baada ya Kenya
Nchi nyingine kama Poland nayo imeweza kuingia katika kumi bora za nchi zinazoleta watalii. Vita ya Ukraine inamaanisha watalii kutoka Urusi watakosekana kutokana na vikwazo, watalii kutoka Ukraine watakosekana na watalii kutoka Poland pia kutokana na hali ya wasiwasi
Kanuni iliyotumika kuvutia watalii wa Urusi inaweza tumika kuvutia masoko mengine ambayo wananchi wake wanaonekana wana akiba ya kutosha ya kutumia. Baadhi ya nchi ni pamoja na China, Korea ya Kusini na nchi zingine.
Pia kuna umuhimu wa kuanza kujiweka kwenye nafasi ya utalii wa mikutano. Nafasi hii Tanzania ilikua nayo miaka sita iliyopita, ni muhimu kuanza kuvutia tena. Lakini jitihada hizi zifanyika pamoja na kujenga vivutio vya kitamaduni na burudani katika maeneo ya majiji.
Serikali inaweza kutumia njia mpya za kujitangaza kupitia mitandao ya kijamii, hasa kwa nchi zenye vijana, akiba ya fedha katika wananchi wake. Kuuza utalii kupitia uzoefu mzuri wa watu katika vivutio vyetu na kufanya utalii katika vivutio vyetu kuwa mtindo mpya wa maisha ( lifestyle) hasa kwa nchi zenye kipato.
2 Responses
Asante kwa uchambuzi mzuri…..wengi tulikuwa hatuelewi athari ya mapigano haya
Nikes kwa sekta ya utalii na sekta ya usafirishaji. But hii is not powerfully comparing na hii kiwanda Cha bidhaa za nyumbani cs this is people (customer) sastication in special needs
…Way to overcome
Wizara husika,wadau wautalii,makampuni na wafanyabiashara wa sekta ya utalii kuifanyia sekat yao kwa ubunifi zaidi either serikali kuongeza msaada katika sekta hii,wafanyabiashara,wadau na makampuni ya utalii kuibua aina nyingine ya utalii wenye tija zaidi sio wanyama tyu Tanzania nia hata michezo, event enterntment ,inside border relationship realtion vitu kama hivi tunategemea vikawa Chachu Cha kumentain eco-tiurism.
✓Kwa biashara nikubali na niseme binafsi bodi husika ,wafanyabiashara wakubwa(producers),wafanyabiashara wa kati (Wholesaler)… Hawa wako na ubinasfi means
(-) they expect customer(finally user) being in sales era
——–The era that comprise much inflation of commodities bring less customer sustainability
…Big giant companies failed to assure their company to be bond/close with their customer in this era ; both they act and collaborate in monopoly system because they accelerate on the same coin
…. There swoc analysis no threat in p’ of people cs ziko kwenye most crucial special needs
+We argue your raw materials facilities and production system threatened internal but where is your brand and marketing budget worked zimefunguwa ndani or zimeingia kuchukua malighafi na uzalishaji lakin inflation inabakipale pale vipi kama hiyo budget ingetumia kufanya customer sustainability ratio not to be affected by this issue ? Kwa kuifanya unafuu uleule wabidha?
✓kulikuwa na haja ya kuiweka Miradi ambayo aiadhiriwa na hali basket kubwa na kuacha hili jambo likawa kubwa ? Sekta ya viwanda ya vitu vya nyumbani inaitaji Sehemu na msaada huo! Mafuta ya kupikia yanambadala wake mfano kilimo tyu kinatosha kupunguza athari hizi vp hiyo bajeti ingeziba gepu kubwa sana ? Serikali tunastopisha au kuondoa Miradi mingine kupisha hili tatizo
Madhara
✓Watu wanakwenda kukosa afya ya lishe Bora kutokana na kutomudu na wajasirlamali wadogo Kaa wapika mikate,vitafunwa kukosa viungo vya mapishi bora kwa wateja wap.
Binafsi
Serikali,wamiliki wa makampuni yalioathirika wafanyabiashara na wadau ndio wenye jibu
😂😂Au to ban biashara ya bidhaa za nyumbani zinazouzwa njee to fill our internal customer satisfaction (people)?