The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Serikali ya Zanzibar Yaja na Ufumbuzi wa Tatizo la Mafuriko Eneo la Mfenesini 

Ni ujenzi wa msingi wa kupitishia maji katika eneo la Mfenesini, kisiwani Unguja, ili kuondoa kero kwa wananchi wa eneo hilo ambao makazi yao huathirika kila ifikapo kipindi cha mvua za masika.

subscribe to our newsletter!

Zanzibar. Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar inatarajia kuanza ujenzi wa msingi wa kupitishia maji katika eneo la Mfenesini, kisiwani Unguja, ili kuondoa kero kwa wananchi wa eneo hilo ambao makazi yao huathirika kila ifikapo kipindi cha mvua za masika.

Mwaka 2021, familia zaidi ya 100 ziliripotiwa kuathirika baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko yaliyowalazimu wakaazi wa eneo hilo kuhama makazi yao. Mafuriko hayo yaliibuka baada ya kupitishwa ujenzi wa barabara mpya iliyojengwa kutoka Bububu hadi Mkokotoni.

Ili kupata ufafanuzi zaidi kuhusu utaratibu wa ujenzi wa msingi wa kupitisha maji, The Chanzo imefanya mahojiano maalum na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Amour Hamid Bakari na hapa anaeleza dhamira ya ujenzi wa msingi huo:

Amour Hamid Bakari: Msingi ule kwa kipindi kirefu umekuwa ni changamoto kubwa kwa wananchi ambao wanaishi katika maeneo yale baada ya kuwa na mradi mkubwa ule wa ujenzi wa barabara ya Bububu mpaka Mkokotoni.

Kumetokea athari kwa baadhi ya maeneo na wizara hivi sasa inatekeleza maelekezo ya Serikali kuhakikisha kwamba maeneo yale yote ambayo yameathirika na ujenzi wa barabara ile au na barabara nyengine pia kufanya utaratibu wa kuyaondosha maji ambayo yanaleta athari kwa wananchi.

The Chanzo: kuna tathmini gani ya utambuzi iliyofanyika mpaka sasa?

Amour Hamid Bakari: Kwanza tulifanya kazi ya kuyatambua maeneo hayo, na hivi sasa maeneo yale yote tumesha yatambua na hivi sasa tunataka kuanza kazi ya ujenzi wa msingi ambao utaondosha maji yanayoingia katika majumba ya wananchi katika eneo la Mfenesini.

Matayarisho yote ya ujenzi wa msingi ule tayari yamekamilika kwa sababu tulitangaza zabuni, baada ya kutangaza zabuni tukapata wazabuni, tukatekeleza matakwa ya sheria, sheria ya manunuzi na uondoshaji wa mali za umma.

Na baadae tukampata yule ambae ni mjenzi na hivi sasa mjenzi yule tayari tumeshafika sehemu kubwa kidogo hata mkataba tumesha saini.

The Chanzo: Ujenzi huu wa msingi wa maji unatarajiwa kuanza lini na kukamilika lini?

Amour Hamid Bakari: Kuna taratibu chache tu ambazo sasa hivi tunasubiri kuzikamilisha ili ujenzi uule uanze. Kwa hiyo, wakati wowote kuanzia sasa msingi ule utaanza kujengwa.

Ukiliangalia lile eneo lenyewe kwa kweli liko kama ni kama shimo ambalo kulikuwa hayo maji yakituama kwa muda mrefu hata kabla ya ujenzi hule. Lakini baada ya ule ujenzi utuamaji wa maji katika eneo lile umeongezeka kwa sababu yale maji sasa yanapata njia na mengi yanakwenda katika eneo lile. Kulikuwa kuna chaguzi tatu za kujenga mtaro ule na kwakweli chaguzi zote ni ngumu.

Tumekwenda na wataalamu wetu, tumekwenda na wakandarasi, tumeshauriana na Serikali ya wilaya, Wilaya ya Magharibi A, kuzitizama chaguzi zote tatu za kuweza kuondosha msingi hule.

Moja ilikuwa tuipitishe kwenye barabara ambayo ile barabara tuichimbe na tupitishe msingi lakini masafa yangekuwa marefu sana, ambayo na gharama zake zingeweza kuongezeka kwa kiasi kikubwa sana.

Tumekubaliana kwa ushauri wa wataalamu wetu, tumekubaliana kuna eneo ambalo tutapitisha ule msingi. Kweli kuna baadhi ya nyumba zitaathirika kutokana na ujenzi wa msingi huo na kuna baadhi ya vipando vya wananchi navyo pia vitaathirika.

The Chanzo: Kuna taarifa yoyote kwa wananchi juu ya ujenzi huu utakaopika katika makazi yao?

Amour Hamid Bakari: Tumeanza kuwataarifu wananchi kupitia Serikali ya wilaya ili kuwambia ile hali iliyokuwepo pale na hasa wenyewe wananchi wanafahamu kwa sababu mimi binafsi nimekuwa nikipokea simu haipiti wiki.

Kwa mfano kama sasa hivi tunaelekea masika hata jana pia nimepokea simu kutoka kwa wananchi wa Mfenesini wanaulizia lini msingi hule utajengwa.

The chanzo: Kuna tathmini gani ya malipo kwa waathirika ambao nyumba zao zitalazimika kuvunjwa kupisha ujenzi?

Amour Hamid Bakar: Tulifanya tathmini ya nyumba zote ambazo tunadhani zitaathirika kutokana na ujenzi wa ule msingi pamoja na vipando vyote, na tathmini hiyo tunayo na hivi karibuni tumeifanyia mapitio tena kuangalia kujiridhisha kama tuliifanya sahihi.

Na ripoti yake tayari imeshakuja na hivi sasa taratibu za ndani za wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha tunatazama namna gani tutaweza kulifanyia kazi hili katika suala zima la makazi ya watu ambayo yataathirika katika lile eneo.

Tulipofanya tathmini, kwa mafano, tulipita katika baadhi ya maeneo ambayo kuna mashina ya muhogo lakini hivi sasa baada ya kufanya mapitio tukakuta kwamba mashina yale ya muhogo hayapo. Kwa hiyo, huwezi ukasema tena ukalipe kitu ambacho sasa hivi hatuto kiathiri.

Lakini pia kuna baadhi ya [miti ya] mivinje ilikuwepo katika lile eneo ambalo tutapitisha ile tathmini, kwa mujibu wa ripoti hii ya mwisho niliyoipata, lakini mivinje ile sasa hivi imekatwa. Kwa hiyo, huwezi ukasema tena tukalipe mtu mwenyewe kashakata mvinje wake kama kauza kama katumia kwa matumizi yake ukasema sasa hivi tukalipe. Hiyo ndio dhamira ya kufanya mapitio ili kujiridhisha.

Hata tutakapoanza ule ujenzi pia tutafanya mapitio tena tukiwa tuko pale kwenye eneo la ujenzi. Kwa sababu tunajua kuna baadhi ya wengine vipando inawezekana watu wakawa wameshavuna vipando vyao. Kwa hiyo, itakuwa haviwezi kuingia katika utaratibu wa malipo.

The Chanzo: Ni njia gani za malipo ambao zitatumika kuwalipa fidia wananchi waliolazimika kuondoa mazao yao pamoja na majumba yao?

Amour Hamid Bakari: Hatujajua kama tutaweza kulipa pesa taslimu au tutatumia utaratibu mwengine. Lakini hapa tunachokizungumza ni kwamba tutahakikisha wale wote ambao watakuwa wameathirika na uule ujenzi wataingia kwenye huu utaratibu ambao Serikali itaamua.

The Chanzo: Ni kiasi gani cha fedha ambacho Serikali imeingia mkataba na mzabuni?

Amour Hamid Bakari: Kwa sabau tulipo itangaza hile zabuni tulikuja na utaratibu wa kufanya michoro na kujenga. Kwa hiyo, ile fedha itakuja tutaitambua rasmi pale tutakapoanza kutaka kufanya hule ujenzi.

Na hasa ukizingatia kwamba lile eneo kama lilivo. Kwa hiyo, huwezi kuja na thamani ya fedha sasa na kama nilivyosema kwamba kulikuwa kuna ugumu mkubwa wakwamba kufikiria wapi tutapitisha maji yale ambayo ni mengi na yanaleta athari kubwa kwa wananchi.

Kwanza nawashukuru kwa ustahamilivu wao waliopata na athari ambazo wanazipata hasa katika kipindi cha mvua kinapo kuja. Lakini kwa wale ambao hawajafikiwa na ujenzi wa aina hii nawaomba wawe na subra Serikali yao sikivu s inaona kwamba changamoto hizi zinawapata.

The Chanzo: Je, ujenzi unatarajiwa kujengwa kuepusha mafuriko ni huo wa Mfenesini pekee au kuna sehemu nyengine?

Amour Hamid Bakari: Tumeanza msingi huu wa Mfenesini tukitoka hapo, siwezi kusema leo, lakini tukitoka hapo tunaenda kwenye msingi mwengine hatua kwa hatua na tutahakikisha maeneo yote ambayo yanaingiliwa na maji kuweza kuyafanyia utaratibu maji yale yasiweze kuingia kwa wananchi.

Salim Khamis ni mwandishi wa The Chanzo kutoka Zanzibar. Anapatikana kupitia salimkombo437@gmail.com

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *