Serikali ya Zanzibar Yaja na Ufumbuzi wa Tatizo la Mafuriko Eneo la Mfenesini

Ni ujenzi wa msingi wa kupitishia maji katika eneo la Mfenesini, kisiwani Unguja, ili kuondoa kero kwa wananchi wa eneo hilo ambao makazi yao huathirika kila ifikapo kipindi cha mvua za masika.
Ofisi ya Mufti Zanzibar: Vitendo vya Udhalilishaji Watoto Vinahuzunisha

Ofisi hiyo inahusisha vitendo hivyo na ushawishi wa shetani na watu kukosa hofu ya Mungu.
Serikali, Wafanyabiashara Wavutana Zanzibar Kuhusu Utoaji wa Stakabadhi Kielektroniki

Mfumo huo wa utoaji stakabadhi umeanza utekelezaji kwenye mwaka unaendelea wa fedha wa 2021/2022 hapo Julai 1, 2021, na kuja kupata umaarufu zaid mwanzoni mwa mwezi Februari 2022 baada ya mamlaka husika kuanza ufuatiliaji wa kuhakikisha wafanyabiashara wanatumia mfumo huo.
Serikali, Wadau Waeleza Mikakati ya Kuboresha Kilimo cha Mwani Zanzibar

Serikali visiwani humo inapanga mikakati ya kuwawezesha wakulima kupanda mwani kwenye maji ya kina kirefu ili kukwepa athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayoripotiwa kudumaza mwani unaolimwa kwenye maji madogo.
Malalamiko Zaidi ya 7,000 ya Wananchi Yamfikia Mwinyi Kupitia App ya Sema na Rais

Mfumo huo ambao ulizunduliwa rasmi mnamo Februari 27, 2021, ulilenga kumsogeza Rais Mwinyi karibu zaidi kwa wananchi ili aweze kusikia moja kwa moja kutoka kwao kero zinazowasumbua na hivyo kuzitafutia ufumbuzi wake.