The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Hospitali ya Benjamin Mkapa Kutafiti Sababu ya Ongezeko la Tatizo la Mawe ya Figo Kanda ya Kati

Wananchi wanabainika kuwa na mawe kwenye figo wanasikia maumivu makubwa sana pembeni ya tumbo karibia na mgongo

subscribe to our newsletter!

Dodoma. Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kati Benjamin Mkapa BMH inatarajia kufanya  tafifiti kubaini sababu ya ongezeko la tatizo la mawe ya figo kwa wakazi wa kanda ya kati inayojumuisha mikoa ya Dodoma, Singida na maeneo ya karibu.

Haya yamebainishwa Agosti 01,2023 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo Dkt. Alphonce Chandika wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya hospitali ya Benjamin Mkapa na mwelekeo wake kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Dkt. Chandika amesema kwa mwaka 2022/2023 kupitia huduma ya uvunjaji wa mawe kwenye mfumo wa mkojo kwa kutumia miale wameweza kutibu wananchi 256.

“Kuna wananchi wanabainika kuwa na mawe kwenye figo wanasikia maumivu makubwa sana pembeni ya tumbo karibia na mgongo.” amesema Dkt. Chandika.

“Na wamekuwa wakija hospitalini na kubainika kwamba kuna mawe yamejitengeneza kule . Tunapata wananchi wengi kutoka nchi nzima, lakini tatizo hili limebainika kuwa kubwa kanda ya kati.”

Dkt. Chandika amesema, wengine wanafiriki huenda ni hali ya hewa ya ukame na wengine kutokunywa maji ya kutosha.

“Tunatarajia kufanya baadhi ya tafiti kujiridhisha kwanini [kanda ya kati]. Wengine wanafikiri ni kwa sababu ya hali ya hewa ya ukame [na] wengine watu kutokunywa maji ya kutosha. Inasababisha ile chumvi chumvi kule inatengeneza vijiwe na inaendelea kukua na kusababisha matatizo makubwa.”

Mawe kwenye figo yanaweza kusababishwa na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na chakula, uzito wa ziada wa mwili, hali fulani za matibabu, na baadhi ya virutubisho na dawa. Mawe yanaweza kuathiri sehemu yoyote ya njia ya mkojo, ikiwa ni pamoja na figo na kibofu.

Hospitali ya BMH imeendelea kujidhatiti katika utoaji wa huduma mbalimbali za kibingwa ikiwemo upandikiza wa figo ambapo watu nane wamepandikizwa figo katika hospitali hiyo.

Pia katika mwaka 2022/23 baada ya hospitali hiyo kupata mtambo maalum wa kuchunguza na kubaini magonjwa ya moyo waliweza kutibu magonjwa ya moyo kwa watoto waliozaliwa na matundu kwenye moyo.

Watoto wawili waliozaliwa na matundu yalizibwa pasipo kufungua kifua na watoto 14 waliobainika kuwa na matundu kwenye moyo walifanyiwa upasuaji kwa kufungua kifua na kuziba.

Katika mwaka huu wa fedha kiasi cha shilingi bilioni 64.5 kimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika hospitali hiyo ili kupunguzia wananchi adha ya kusafiri mbali kupata matibabu.

Maendeleo hayo ni pamoja na kuendeleza ujenzi wa jengo la Saratani, ambapo mpaka sasa limefikia asilimia 27. Eneo lingine ni ujenzi wa jengo la matibabu ya moyo na kifua kwa watoto na watu wazima.

Hospitali ya Benjamin Mkapa inahudumia wananchi milioni 10 wa mikoa ya Dodoma, Iringa, Singida, Manyara na baadhi ya maeneo ya mikoa ya Mogorogo na Tabora.

Jackline Kuwanda ni mwandishi wa habari wa The Chanzo anapatikana mkoani Dodoma unaweza kumpata kupitia jackline@thechanzo.com

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *