The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Tume Yaitaka Serikali Kuacha Kuanzisha Taasisi Zenye Taswira ya Kijeshi

Yasema utaratibu huo hukwamisha utekelezaji wa haki jinai nchini.

subscribe to our newsletter!

Dar es Salaam. Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai Tanzania imemshauri Rais Samia Suluhu Hassan kusitisha utaratibu wa kuanzisha taasisi zenye taswira ya kijeshi nchini, ikisema utaratibu huo unachangia kuzorotesha hali ya upatikanaji wa haki jinai kwa wananchi.

Kwenye muhtasari wa ripoti yake iliyoiwasilisha kwa Rais Samia hapo Julai 15, 2023, tume hiyo iliyofanya kazi yake chini ya uenyekiti wa Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman imeanisha changamoto kadhaa zinazotokana na uwepo wa vyombo vya haki jinai vinavyotekeleza majukumu yake kwa taswira ya kijeshi.

Changamoto hizi ni kama vile matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya watuhumiwa katika ukamataji; upekuzi na mahojiano; ubebaji na matumizi ya silaha za kivita; uvaaji wa vyeo vinavyoshabihiana na vyeo vya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ); na taasisi kujilinganisha hadhi na JWTZ, zikiwemo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jeshi la Uhamiaji na Jeshi Usu la Uhifadhi.

SOMA ZAIDI: Tume Yataka Uchunguzi Mali Zilizotaifishwa Chini ya Utaratibu wa Kukiri Kosa

“Utitiri wa vyombo vyenye taswira ya kijeshi umesababisha taasisi zenye sura ya kijeshi kuwa nyingi, taasisi za haki jinai kukosa ushirikiano kutoka kwa wananchi kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya wananchi juu ya kunyanyaswa na kuteswa na taasisi zenye taswira ya kijeshi, na kuwepo kwa uwezekano wa kusambaa kwa silaha, suala linaloweza kutishia amani nchini,” tume hiyo imebainisha.

Tume imeshauri kwamba shughuli za Zimamoto zigatuliwe kwenda Serikali za Mitaa ili kuzifanya huduma za zimamoto ziwe karibu na wananchi. Vilevile, ugatuzi huo utasaidia kufungamanisha shughuli za zimamoto na uokoaji na shughuli za mipango miji ambazo hutekelezwa na Serikali za Mitaa, Tume imeona.

Mapendekezo mengine ya Tume kuhusiana na suala husika ni kama yafuatayo:

  • Taasisi ambazo zinatekeleza majukumu ya Haki Jinai, au zinazotoa huduma kwa wananchi zenye taswira ya kijeshi, mathalani Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jeshi la Uhamiaji na Jeshi Usu la Uhifadhi wa Wanyamapori na Misitu, zirejee katika majukumu yake ya awali ya utoaji wa huduma kwa wananchi.
  • Huduma za Zimamoto na Uokoaji zirejeshwe na kutekelezwa katika ngazi za halmashauri hasa ikizingatiwa shughuli za zimamoto zina muingiliano mkubwa na shughuli nyingine za halmashauri katika mipango miji.
  • Mafunzo kwa Askari wa Uhifadhi wa Misitu na Wanyamapori yatolewe na Jeshi la Polisi kwa kuzingatia misingi ya Haki za Binadamu na utawala wa Sheria.
  • Wizara ya Maliasili na Utalii iwarejeshe watumishi wote raia katika vyeo vyao vya ajira ya awali na kuwaondolea mavazi na vyeo vya kijeshi isipokuwa mavazi yavaliwe na watumishi walioko kwenye Idara inayohusika na majukumu ya kupambana na ujangili.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *