The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Utata wa Kisheria Waibuka Rais Samia Akimrudisha Mwenyekiti Aliyemuondoa TCRA

Baada ya Dkt Killimbe kumaliza kipindi chake cha miaka minne, Rais Samia alimteua tena kwenye nafasi hiyo kuanzia Aprili 19, 2021. Dk Kilimbe alidumu kwenye nafasi hiyo mpaka Septemba 18, 2022, ambapo uteuzi wake ulitenguliwa.

subscribe to our newsletter!

Rais Samia Suluhu Hassan amemrudisha Dk Jones A Killimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), akiibua maswali kadhaa ya kisheria miongoni mwa wadadisi wa mambo nchini.

Uteuzi huu unakuja ikiwa ni takribani miezi 14 toka Dk Killimbe aondolewe kwenye nafasi hiyo nyeti, akirithiwa na Othman Sharif Khatib.

Katika uteuzi huo uliotangazwa leo Novemba 13,2023, Juma Hassan Reli ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TCRA.

Dk Killimbe, ambaye ni mtaalamu mbobezi wa masuala ya mawasiliano aliyefanya kazi ndani ya nchi na hata na mashirika ya kimataifa, aliteuliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA Novemba 17, 2016.

Baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka minne, Rais Samia alimteua tena kwenye nafasi hiyo kuanzia Aprili 19, 2021. Dk Kilimbe alidumu kwenye nafasi hiyo mpaka Septemba 18, 2022, ambapo uteuzi wake ulitenguliwa.

Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano inaeleza kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TCRA atahudumu kwa kipindi cha miaka minne. Sheria inaeleza zaidi kuwa Mwenyekiti na Makamu wake wanaweza kuteuliwa tena katika kipindi kinachofuatana.

Baadhi ya wadadisi wamehoji kwamba ingawa Dk Kilimbe hakumaliza kipindi cha miaka minne katika uteuzi wake wa pili, uteuzi wake wa mara ya tatu, unafanyika kukiwa tayari kuna Mwenyekiti mwingine aliyeshika hatamu.

Wakosoaji wanatumia hoja hii kubainisha kwamba uteuzi wa Dk Kilimbe haujafanyika katika vipindi vinavyofuatana, au ‘successive term’ kwa kimombo kama sheria inavyotaka.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *