Kampuni ya Facebook imetoa taarifa kwa wateja wake kuwa kuanzia Disemba 1,2023, matangazo ya Facebook yatatozwa kodi ya VAT, ambayo ni asilimia 18 ya thamani husika. Facebook imewataka wateja wote wanaotumia huduma za matangazo ya Facebook kujisajili kwa kuwasilisha namba zao za VAT katika mfumo wa Facebook.
“Kuanzia Disemba 01,2023, matangazo ya Facebook Tanzania yatakuwa yanatozwa kodi ya VAT,” imeeleza taarifa hiyo iliyotumwa na kampuni ya Meta, kampuni mama ya mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram, Thread na WhatsApp.
Katika taarifa yake, Meta imeeleza kuwa, wateja wa Facebook wenyewe ndio watakaohusika na ulipaji wa kodi hiyo, baada ya kujikadiria na kwamba Facebook hawatafanya makato ya moja kwa moja.
Mnamo Julai 2023, serikali ilifanya mabadiliko ya sheria ya kodi ili kuruhusu serikali kukusanya VAT hata kwa makampuni yasiyo na ofisi nchini, hasa yale yanatoa huduma za kidigitali. katika mabadiliko haya serikali inategemea kukusanya Bilioni 34.
Serikali pia ilianzisha kodi ya mapato ya asilimia 2 kwenye malipo yanayofanywa kwa watoa huduma za kidijitali wa kigeni. Serikali inategemea kukusanya walau Bilioni 4.8 kupitia kodi hii mpya.
Ili kuiwezesha Mamlaka ya Mapato kuweza kukusanya kodi hizi, Mamlaka ilianzisha mfumo wa mtandao ambapo watoa huduma mbalimbali wa kidigitali wamehimizwa kujiunga ili kutimiza matakwa ya kisheria.
One Response
Napataje Hio vat tax, ila tin. No. Ninayo tayali naomba msaada ili nijaze taarifa zangu Facebook.