The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Ripoti Ya Haki Za Binadamu 2023: Matukio Ya Watu Kujiua Yameongezeka, Wengi Wanaojiua Ni Wanaume Vijana

Sehemu kubwa ya waliojiua ni vijana wa umri kati ya miaka 18 mpaka 35 ambapo walikua asilimia 46, huku ikifuatiwa na watu wenye umri miaka 36 mpaka 59 ambapo walikua asilimia 27. Kwa ujumla asilimia 71 ya matukio ni watu wenye umri chini ya miaka 35.Ripoti inaeleza zaidi kuwa sehemu kubwa ya watu waliojiua ni wanaume, hasa vijana.

subscribe to our newsletter!

Ripoti ya haki za binadamu kwa mwaka 2023 iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu inaonesha matukio ya watu kujiua yameongezeka kwa mwaka 2023. Ripoti inaonesha wakati kwa mwaka 2022, watu 22 walijiua kwa mwaka 2023, Kituo kilirekodi matukio 57 ya watu kujiua.

Sehemu kubwa ya waliojiua ni vijana wa umri kati ya miaka 18 mpaka 35 ambapo walikua asilimia 46, huku ikifuatiwa na watu wenye umri miaka 36 mpaka 59 ambapo walikua asilimia 27. Kwa ujumla asilimia 71 ya matukio ni watu wenye umri chini ya miaka 35.Ripoti inaeleza zaidi kuwa sehemu kubwa ya watu waliojiua ni wanaume, hasa vijana.

Uchambuzi wa ripoti hiyo unaonesha watu walijiua kwa sababu mbalimbali ikiwemo madeni, kutelekezwa, kukosa ada, kuiga matukio kutoka katika filamu za kuigiza, mapenzi, ukali wa wazazi, wivu, kuachishwa kazi na ugumu wa Maisha.

Ripoti inahusisha matukio haya na suala zima la afya ya akili. Huku ikieleza baadhi ya changamoto kama kukosa ajira na makuzi katika familia kuwa mizizi ya matatizo haya.

Ripoti inaonesha baadhi waathirika hutokea katika familia ambazo  wazazi wao wameingia katika majukumu ya familia wakiwa hawajapevuka na hivyo kupata msongo ambao husababisha watoto wanaowalelea pia kuathirika moja kwa moja.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *