The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Familia Yahaha Mwezi Mmoja Ukikatika Toka Mfanyabiashara wa Mkonge Tanga Atoweke

Enock John Chambala (41) ni mfanyabiashara wa Mkonge huko jijini Tanga anasemekana kutoweka toka Julai 06,2024

subscribe to our newsletter!

Familia ya Enock John Chambala (41) imeendelea kujawa na hofu juu ya hatma ya ndugu yao aliyetoweka katika mazingira ya kutatanisha toka Julai 06,2024.

Chambala ni mfanyabiashara wa zao la Mkonge mwenye makazi yake mkoani Tanga, katika mtaa wa Kange.Toka Julai 06,2024, familia ilianza kuingiwa na wasiwasi baada ya Chambala kutopatikana katika simu yake.

Mdogo wake Chambala, Baraka John Chambala aliamua kuchukua jukumu la kufika nyumbani kwa Chambala ikiwemo kuuliza kwa ndugu na marafiki ikiwa wanafahamu alipo mfanyabiashara huyo.

Mazingira yaliyokutwa nyumbani kwake kwa mujibu wa mdogo wake ni kama mtu aliyeondoshwa bila hiari yake huku akiacha chakula na jiko likiwa linapasha chakula taratibu. Mdogo wake anaeleza pia kuwa walikuta mlango wa nyumba yake ukiwa haujafungwa, jambo ambalo sio kawaida kwa Chambala.

Kutokana na mazingira kuonekana yamejaa utata, familia iliamua kufungua shauri katika kituo cha Polisi Tanga na kupewa RB no. TAN|RB|3040|2024, hata hivyo hakuna dalili zozote za kuonesha ndugu yao yupo wapi na kama yu mzima au la.

Hivi karibuni kumekuwa na matukio mengi ya watu kupotea, huku wengine wakitekwa. Jeshi la Polisi na Serikali limeeleza kuwa sio matukio yote ni ya utekaji, na pia kukanusha taarifa zilizokuwa zikihusisha vyombo vya usalama na matukio ya utekaji wa Watanzania.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *