Kesi namba 1883/2024,inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda imeharishwa hadi mwezi septemba 2024 baada ya kuelezwa kuwa hakimu anayehusika kusikiliza kesi hiyo Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza, Erick Marley anakabiliwa na tatizo la kiafya.
Akizungumza mara baada ya kuahirisha kesi hiyo hakimu mkazi mfawidhi wa Wilaya ya Ilemela Stella Thomas Kiama, ameeleza kuwa kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena terehe 10,11 na 12 mwezi Septemba mwaka huu. Aidha licha ya mdhamini na mawakili wake kufika mahakamani hapo, mshtakiwa hakuwa wamefika.
Dk Nawanda alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Jumanne Julai 9, 2024, ambapo alisomewa shtaka moja la kulawiti kinyume na kifungu namba 154 (1) (a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16, shtaka ambalo alilikana.
Aidha Jumanne Julai 16, 2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza, Erick Marley kesi hiyo ilizikizwa tena kwa mara ya pili ambapo mashahidi wawili wa upande wa mashtaka walisikizwa na kisha kesi kuahirishwa hadi leo August 13, 2024.
Nawanda anashtakiwa kwa kosa la kumwingilia kinyume na maumbile ‘kumlawiti’ Tumsime Ngemela, kosa alilolitenda Juni 2, 2024 eneo la maegesho ya magari, lililoko Rock City Mall wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
Taarifa ya mwanafunzi huyo kudaiwa kulawitiwa ziliripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari Juni 11, 2024 na kupelekea uteuzi wake kutenguliwa asubuhi ya siku hiyo na Alhamisi Juni 13, 2024 jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza lilithibitisha kumshikilia nawanda kwa tuhuma za ulawiti.