The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Mvutano wa Kisheria Waanza Kesi ya Boniface Jacob, Andiko Kuhusu Mafwele Lawekwa Kwenye Hati ya Mashtaka

Upande wa mashtaka pia umeiomba Mahakama isimpe Boniface Jacob dhamana kwa kueleza kuwa usalama wake upo hatarini. Jambo ambalo mawakili wake wameeleza halina msingi wowote wa kisheria.

subscribe to our newsletter!

Boniface Jacob ameweza kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Septemba 19,2024,toka akamatwe hapo jana katika mgahawa wa Golden Fork, Sinza.

Hati ya Mashtaka ya kesi inayomkabili Boniface Jacob inaeleza kuwa anatuhumiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo kinyume na Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, kifungu cha 16.

Katika shitaka la kwanza linaeleza kuwa Boniface Jacob mnamo Septemba 12, 2024, akiwa Dar es Salaam alichapisha taarifa za uongo zikieleza kuwa: “…Mafwele anatuhumiwa na familia nyingi kama mtu ambaye ameshiriki mauaji kwa moja katika kuwapoteza ndugu wa baadhi ya familia zao; kupotea kwa Mfanyabiashara Mussa mziba, Kupotea kwa Deo Mugasa, Kupotea kwa Adinani Hussein Mbezi, Kupotea kwa vijana watano wa Aggrey..” katika mtandao wa X (zamani uliojulikana kama X0 akitumia jina la Boniface Jacob@ExmayorUbungo akikusudia kuudanganya umma.

Na shitaka la pili pia linahusu kuchapisha taarifa za uongo kinyume ambapo linaeleza: Boniface Jacob mnamo Septemba 14,2024, alichapisha taarifa za uongo zilizosema;”….Mkawasifia maRCO wanaouzuia uhalifu kwa kutenda uhalifu,…Bali Ma RCO waliojua kuteka, kukamata, kupiga watuhumiwa risasi, kuwafunga tape, kuwafunga mifuko ya nailoni usoni na kisha kutupa miili ya watuhumiwa ndiyo wanaojua kazi ya upolisi…” katika mtandao wa X (zamani uliojulikana kama Twitter) akitumia jina la Boniface Jacob@ExmayorUbungo akikusudia kuudanganya umma.

Jacob aliyakana mashtaka yote mawili katika kesi hiyo anayowakilishwa na Mawakili watatu akiwemo Peter Kibatala na Hekima Mwasipu.

“Upande wa mashtaka umeleta maombi wanataka Mahakama imuamuru Boni awape maafisa wa polisi wapelelezi, wachunguzi uwezo wa kuingia kwenye simu yake na mtandao wa X. Kwa hiyo tumepinga vikali maombi hayo tumesema hayana sababu , wala msingi wowote kisheria,” alieleza Wakili Kibatala akizungumzia mwenendo wa kesi hiyo.

Upande wa mashtaka pia umeiomba Mahakama isimpe Boniface Jacob dhamana kwa kueleza kuwa usalama wake upo hatarini. Jambo ambalo mawakili wake wameeleza halina msingi wowote wa kisheria.

Maamuzi kuhusu dhamana ya Boniface Jacob yanategemewa kutolewa mnamo Septemba 23, 2024, saa tano asubuhi.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *