Chama cha ACT Wazalendo kimeripoti leo Disemba 01,2024, kuwa Mwenyekiti wake wa Ngome ya Vijana, Abdul Mohamed Nondo ametekwa asubuhi ya leo akitoka mkoani Kigoma.
“Mashuhuda wa tukio wanasema kuwa kulikuwa na purukushani katika utekaji wa Nondo hali iliyosababisha begi lake dogo kudondoka,” inaeleza taarifa hiyo iliyotolewa na Mbarala Maharagande, Naibu Katibu wa Haki za Binadamu na Vyombo vya Uwakilishi wa Wananchi, ACT Wazalendo.
Taarifa hiyo inaeleza zaidi kuwa Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo Mkoa wa Dar es salaam Monalisa Ndala na Afisa wa Harakati na Matukio Taifa Wiston Mogha walipofika kituoni hapo walitambua kuwa aliyetekwa ni Nondo kwa sababu walizitambua nguo zake kwenye begi lililodondoka na note book yake.
Tukio la utekaji liliwahi kumkumba Nondo mnamo Machi 2018, ambapo alikamatwa na watu waliomsafirisha kutoka Dar es Salaam mpaka Mafinga, wakati huo akiwa mwanafunzi wa chou.
ACT Wazalendo imetoa wito kwa Polisi kufuatilia na kuhakikisha