The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

China, Zambia na Tanzania Kuingia Mkataba wa Uwekezaji wa Trilioni 3.6 Kwa Kampuni ya China CCECC Kuendesha TAZARA kwa Miaka 30

Kwa upande wa China reli ya TAZARA ina umuhimu mkubwa hasa katika usafirishaji wa madini muhimu kutoka DR Congo na Zambia, maeneo ambayo China ana uwekezaji mkubwa. TAZARA pia ni muhimu kwa China hasa katika ushindani wake na Marekani

subscribe to our newsletter!

Mazungumzo ya uwekezaji katika reli Tanzania na Zambia (TAZARA) yapo katika hatua za mwisho ambapo kampuni ya China, China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) inatarajiwa kuwekeza dola Bilioni 1.4 katika reli hiyo na kuiendesha kwa miaka 30.

Haya yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa reli ya TAZARA, Bruno Ching’adu katika mkutano wa wawekezaji wa madini na nishati (ZIMEC 2025) uliofanyika Kitwe nchini Zambia.

“Uwekezaji kutoka CCECC hautairejesha tu miundombinu yetu ya reli, bali pia utaifanya TAZARA kuwa mwezeshaji muhimu wa biashara na ukuaji wa uchumi kati ya Tanzania na Zambia,” ameeleza Mhandishi  Ching’andu.

Katika makubaliano hayo ya nchi tatu, CCECC itawekeza dola bilioni 1 katika ukarabati wa reli ya TAZARA, na dola milioni 400 zitatumika katika kununua vichwa 32 vya treni, pamoja na mabehewa ya mizigo 762. Katika miaka 30 ya uendeshaji; miaka mitatu ya mwanzo itatumika katika matengenezo na miaka 27 itatumika katika uendeshaji rasmi wa reli hiyo.

Mazungumzo ya uendeshaji wa reli hii yalianza kufuatia kudorora kwa utendaji wa reli hii na hasara za muda mrefu. Ambapo mazungumzo rasmi yalifanyika kuanzia mwaka 2016, hata hivyo baadae yalivunjika huku baadhi ya ripoti zikionesha mfupa mgumu ulikua ni deni la TAZARA na masuala ya kikodi.

Mazungumzo yalirudi rasmi baada ya kipindi kirefu na mnamo Disemba 12, 2023, wataalamu kutoka China walitumwa kwa ajili ya ukaguzi wa reli hiyo yenye kilomita 1,860. Baada ya hapo, maongezi yalianza Mei 2024 na mnamo Septemba 2024, katika kikao cha Marais wa China, Tanzania na Zambia huko mjini Beijing, makubaliano ya nchi hizi tatu yalisainiwa juu ya reli hii.

Umuhimu wa TAZARA

Kwa upande wa China reli ya TAZARA ina umuhimu mkubwa hasa katika usafirishaji wa madini muhimu kutoka Zambia na hata DR Congo, maeneo ambayo China ana uwekezaji mkubwa. TAZARA pia ni muhimu kwa China hasa katika ushindani wake na Marekani, ambapo kwa sasa Marekani anajipanga  kujenga reli itakayopita Angola, ikiunganisha DR Congo na Zambia, huku ikielekea bahari ya Atlantic.

Hii ikimaanisha kuna ushindani mkubwa juu ya njia za usafiri, yaani kupitia Tanzania (bahari ya hindi), au kupitia bahari ya Atlantiki, huku nchi zote zikiangalia madini muhimu yanayopatikana DR Congo na Zambai. DR Congo na Zambia ni wateja wakubwa wa bandari ya Dar es Salaam, ikimaanisha kuimarika kwa njia za kupitisha mizigo hasa reli, kutaiwezesha bandari za Tanzania kuwa na biashara zaidi.

Kihistoria reli ya TAZARA, ni mradi mkubwa wa kwanza China kuufanya katika nchi za Afrika, na pia ni mradi mkubwa wa kwanza katika sera yake ya mambo ya nje, toka kufanyika mapinduzi ya mwaka 1949 yalioanzisha Jamhuri ya Watu wa China. Mradi huo ambao pia unajulikana kama reli ya Uhuru, uliundwa baada ya Zambia kukabiliwa na vikwazo vikali kutoka kwa serikali za wakoloni, zilizokuwa zikiizunguka, ikiwemo kuhujumiwa katika kusafirisha shaba, bidhaa iliyokuwa ikibeba uchumi wa Zambia.

Tanzania na Zambia zilijaribu kufikia nchi mbalimbali ikiwemo Canada, Marekani na Shirikisho la Sovieti wa ajili ya kujenga reli hiyo, ambapo wote waliona mradi huo hautekelezeki na ni wa kisiasa zaidi.

Baada ya Rais Nyerere kutembelea China na kukutana na kiongozi wa nchi hiyo Mao Zedong mnamo Februari 1965, China ilionesha dhamira ya kujenga reli hiyo na mnamo Septemba 05, 1967,mkataba rasmi ulisainiwa. Mwezi Machi 1968, mamlaka ya kuendesha reli hiyo TAZARA ilianzishwa. Ujenzi rasmi ulianza Oktoba 1970 na kukamilika mwaka 1976, ambapo mnamo Julai 14, 1976, majaribio rasmi katika reli hiyo mpya yalianza.

Watu 160 walifariki wakati wa ujenzi wa reli hiyo iliyohusisha wafanyakazi 51,500. Hata hivyo, reli hii imeendelea kubakia kuwa alama muhimu ya ushirikiano kati ya Zambia, Tanzania na China, hasa kutokana na kuwa China haikudai malipo ya mkopo uliotoa wa dola milioni 500, katika ujenzi wa reli hii.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×