The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Mazito Yaibuka Ripoti Ya Wafanyabiashara Wa Kigeni Kariakoo: ‘Wako Waliopiga Simu Kuzuia Uchunguzi’

Kampuni kadhaa za wageni zinafanya kazi mtandaoni bila usajili wala leseni, maduka yote 29 yanayofanya kazi mtandaoni yaliyoangaliwa na kamati hayakua na leseni. Kati ya majukwaa 14 ya mtandaoni, 12 hayakuwa na leseni

subscribe to our newsletter!

Kamati maalum iliyohusika na kuchunguza suala la wageni kufanya biashara zinazotakiwa kufanywa na wazawa Kariakoo. Kamati hiyo imewasilisha ripoti hiyo Machi 17, 2025, kwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

Mazito yaliyoibuliwa na kamati ni pamoja na:

  • Kati ya makampuni 9,380 yaliyosajiliwa Brela ni asilimia 9.2 ambazo wamesajiliwa kwenye kituo cha uwekezaji, ‘hali hii inaashiria uwepo wa mianya inayoruhusu wageni kusajiliwa kampuni na kufanya biashara zinazodhaniwa kupaswa kufanywa na wazawa bila ufuatiliaji wa kutosha,’ Kamati.
  • Wageni wanauza bidhaa kwa bei ya chini ya soko hivyo kupunguza uwezo wa wazawa kuhimili ushindani;
  • Wageni wanawaondoa wazawa katika maeneo ya biashara waliyopangisha kwa kulipa kodi kubwa, na kwa kutumia malipo ya ziada yanayojulikana kama kilemba;
  • Wageni kumiliki mnyororo wote wa thamani toka mzigo unapoagizwa mpaka kufika kwa mlaji: Wanaagiza mizigo, na kuitoa bandarini kupitia kampuni za kigeni na kusafirisha kupitia kampuni za kigeni;
  • NIDA za watumishi wa kitanzania wa makampuni ya wageni kutumika kufungua makampuni, huku Watanzania wakionekana kuwa wamiliki wakati ni wafanyakazi tu;
  • Kampuni kadhaa za wageni zinafanya kazi mtandaoni bila usajili wala leseni, maduka yote 29 yanayofanya kazi mtandaoni yaliyoangaliwa na kamati hayakua na leseni. Kati ya majukwaa 14 ya mtandaoni, 12 hayakuwa na leseni;
  • Kamati ilivyoenda kununua bidhaa katika maduka kumi wakati wa uchunguzi, 8 hayakutoa risiti, katika wawili waliotoa risiti, mmoja alitoa ya kughushi;
  • Wafanyabiashara wengi wa kigeni Kariakoo hawatumii benki, wanafanya malipo kwa kubadilishana bidhaa kati yao;
  • Katika maduka 75 yaliyotembelewa na kamati Kariakoo, ilibainika kuwa maduka hayo yameajiri wageni 152, ambapo wageni 148 wanauza bidhaa za rejareja;

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×