Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amekamatwa na Jeshi la Polisi, Mbinga mkoani Ruvuma punde baada ya kumaliza mkutano wake leo April 09, 2025.
“Baada ya mkutano leo jioni saa 12:00 wilaya ya Mbinga, wakati wa kufunga mkutano OCD alimfuata Mwenyekiti Tundu Lissu Jukwani akamwambia tafadhali ukishuka hapo jukwani Ingia kwenye gari ya Polisi nakutaka Polisi kwa mahojiano. Mh Lissu alimwambia nimefanya nini ? Huku akiendelea kuchangisha fedha ktk hadhara ‘ Tone Tone,” ameandika Godbless Lema kwenye ukurasa wake wa X.
“Baada ya kuona hiyo zogo , Kamanda Sosopi alimfuata OCD nakumwambia kama Lissu analo jambo na nyie [tafadhali] mnaweza kuja pale tulipofikia mkamchukua kwa utaratibu hapa mtazua tafrani kubwa maana halaiki hapa ni kubwa, pia mimi nilisisitiza ushauri huo kwa OCD na wasaidizi wake wengine, alionekana kama anaelewa lakini ghafla mabomu ya machozi mengi yalianza kurindima. Mh Lissu amekamatwa na sasa yuko kituo cha Polisi Mbinga,” anaeleza zaidi Lema.
Katika taarifa yake, CHADEMA imeeleza wengine waliokamatwa ni pamoja na Aden Mayala, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kusini, Felius Festo, Mratibu wa Uhamasishaji BAVICHA Taifa, Shija Shebeshi na mlinzi wa Lissu.
Bado jeshi la Polisi halijatoa taarifa rasmi juu ya sabbau za kumshikilia Lissu.
One Response
We enjoy it