The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

 ZEC Yapunguza Gharama za Fomu za Uchaguzi kwa Wanawake Kuhamasisha Ushiriki

ZEC imeeleza kuwa punguzo hilo linakusudia kuongeza ushiriki wa wanawake katika siasa na kupunguza vikwazo vya kifedha vinavyowakwamisha wengi wao.

subscribe to our newsletter!

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza kupunguza nusu ya ada ya kuchukua fomu kwa wanawake watakaowania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Kupitia taarifa iliyosomwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC Radio) Aprili 10, 2025, ZEC imeeleza kuwa punguzo hilo linakusudia kuongeza ushiriki wa wanawake katika siasa na kupunguza vikwazo vya kifedha vinavyowakwamisha wengi wao.

Gharama za awali za ada katika uchaguzi wa mwaka 2020, mgombea wa nafasi ya udiwani alitakiwa kulipa Shilingi 10,000 pamoja na dhamana ya Shilingi 50,000. Nafasi ya uwakilishi ada iliukuwa Shilingi 50,000 na dhamana ya Shilingi 300,000, huku nafasi ya Urais ilihitaji ada ya Shilingi 100,000 na dhamana ya Shilingi milioni mbili.

Kufuatia hatua hiyo ya ZEC Aprili 13, 2025, Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar  (TAMWA-Z), Dk Mzuri Issa, aliipongeza ZEC kwa kuonyesha dhamira ya kuwahusisha wanawake zaidi katika siasa, akibainisha kuwa punguzo hili linafungua milango kwa wanawake wengi wenye uwezo na nia ya kuongoza.

TAMWA Zanzibar imetoa wito kwa wanawake wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hii adhimu, na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao ili kuongeza uwakilishi wa kijinsia katika nafasi za maamuzi.

“Hatua hii ya ZEC ni muhimu kwa kuwa inaangazia moja kwa moja vikwazo vya kihistoria na kijamii vinavyowakwamisha wanawake katika siasa,” amesema Dk Mzuri.

Takwimu za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 zinaonesha kuwa kati ya wagombea 601 waliokuwa wamechukua fomu kuwania nafasi 106 za udiwani na uwakilishi, wanawake walikuwa ni 135 tu. Na wanawake 37 tu ndiyo walioweza kushinda katika uchaguzi huo.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×