The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Kwa Nini Watoto Wadogo Hukosa Usingizi Usiku?

Ratiba ya kulala inayojirudia kila siku ni msaada mkubwa. Tuhakikishe pia kuwa mtoto analala mchana kwa muda unaotosha.

subscribe to our newsletter!

Mara nyingi mchakato wa watoto wadogo kwenda kulala hufanana: Umemuogesha mtoto wako, ukamvalisha nguo zake za kulalia, umezima taa, na ukatoka chumbani ukinyata ukiwa na tumaini kwamba mtoto amelala.

Muda mfupi baadaye mlango unafunguliwa kwa upole. “Mama? Baba? Siwezi kulala.” Kama hili limewahi kukutokea, jua hauko peke yako. Kukosa usingizi kwa watoto wenye umri wa mwaka mmoja hadi mitatu ni jambo la kawaida kabisa na siyo kosa lako na hata si kosa la mtoto. Mara nyingi ni sehemu ya ukuaji wao wa kawaida kabisa.

Watoto wa umri huu hujifunza mambo mengi kwa wakati mmoja: kutembea, kuongea, kuelewa hisia, na hata kupima mipaka. Akili zao huwa hazipumziki hata wanapolala. Ndio maana unaweza kuona mtoto anaonekana amechoka sana, ana dalili zote za usingizi lakini hasinzinzii.

Ratiba tulivu ya kulala inaweza kusaidia sana. Tumia muda wa utulivu kabla ya kulala soma kitabu, imba wimbo wa taratibu, punguza mwanga wa taa chumbani. Mwili na akili vitatambua kwamba ni muda wa kupumzika na atalala.

Kwa mtoto mdogo, “sisi” ni kila kitu. Kuwa mbali na watu wanaomzunguka mchana kutwa, hasa wazazi au walezi, hata kwa saa chache usiku huwapa hofu na maumivu ya kihisia. 

SOMA ZAIDI: Je, ni Kweli Kwamba Malezi ya Sasa Yamekuwa Magumu Kuliko ya Zamani?

Kuanzia miezi 18 na kuendelea, watoto wengi hupitia hali hii kwa sababu wanakuwa wametengeza ukaribu sana na watu hawa wanaoamini uwepo wao ni faraja na usalama wao.

Tujaribu kuwa na utaratibu wa usiku unaojirudia kila siku: busu la usiku mwema au kauli ya upendo. Hii huwapa faraja na kuwasahaulisha kuwa hatupo mbali nao. Pia, tuwe na muda maalum wa wanafamilia wote kwenda kulala hata ikiwezekana kuigiza kama mnaenda wote kulala ili watoto waikariri ratiba hiyo na ikifika muda wa kulala wasisumbue.

Pia, mtoto anaweza ghafla kuanza kusema anaogopa giza, au kivuli, au “kitu” fulani alichosikia au anachokihisi. Akili zao zinapoendelea kukua, ubunifu huongezeka, na ndoto au fikra huweza kuwa chanzo cha hofu. 

Pia, katika umri huu kisayansi ubongo wao huwa unachakata taarifa zote za kutwa nzima na kuzihifadhi katika semu ya ubongo ya kutunza kumbukumbu na pia ubongo huwa unapangiliwa kama hatua ya ukuaji na ukomavu, hivyo hupeleka mishtuko ya ghafla usingizini na hivyo kuwapa hofu na woga.

Tuchukulie hofu hizo kwa uzito, lakini bila kuzipa nguvu. Tutumie mwanga wa usiku kutengeneza mchezo wa kufukuza vivuli vyetu ili wajue kivuli hutokea pale mwanga unapoakisi kitu au mtu wakati wa usiku au mchana. 

SOMA ZAIDI: Wazazi Waliopo Kimwili Lakini Wasiopatikana Kihisia Hukuza Watoto Wasiojali Thamani ya Upendo

Mnaweza kuwaelezea kisayansi kadri wanavyozidi kukua ili waone ni jambo la kawaida na halipaswi kuwatisha. Mambo haya hujenga imani ndani yao na kuamini ukweli kwamba kivuli si kitu au mtu halisi.

Ndiyo, mtoto anaweza kuwa amechoka sana kiasi kwamba hawezi kulala. Kukosa usingizi wa mchana au kuchelewa kulala hupelekea mwili wake kutoa homoni za kuchangamka.

Ratiba ya kulala inayojirudia kila siku ni msaada mkubwa. Tuhakikishe pia kuwa mtoto analala mchana kwa muda unaotosha.

Huu ni wakati wa kusema “hapana” kila mara. Mtoto anajitambua na anajaribu kudhibiti mazingira yake. Na muda wa kulala unakuwa wakati wa mapambano.

Badala ya kulazimisha kila kitu, tuwape chaguo. “Unataka nguo ipi ya kulala?” au “Kitabu gani ungependa tusome leo?” Kumshirikisha katika maamuzi humfanya ajisikie kuthaminiwa na kupunguza migogoro.

SOMA ZAIDI: Wazazi na Walezi, Uelewa Juu ya Mahusiano Yenye Afya ni Muhimu kwa Watoto Wetu

Kelele, mwanga mkali, joto, shuka linamuwasha… mambo haya yanaweza kuathiri usingizi. Tuhakikisha chumba ni tulivu, chenye hewa ya kutosha, mwanga kidogo, na blanketi au shuka laini. inaweza kusaidia.

Sukari, vyakula vizito usiku, na muda mwingi mbele ya runinga, simu, na kadhalika, huweza kuchelewesha usingizi. Tuwape watoto vitafunwa vyepesi kama ndizi au maziwa ya moto kabla ya kulala, na tuepuke kuangalia runinga usiku na watoto wa wadogo.

Mfano wa ratiba bora ya kulala

· 6:30 jioni – Kuoga kwa maji ya vuguvugu

· 6:45 jioni – Kuvaa nguo za kulala na kupiga mswaki

· 7:00 jioni – Kusoma kitabu au kusikiliza hadithi ya taratibu

· 7:15 jioni – Busu, maneno ya upendo, taa kuzimwa

Usiku mwingine utakuwa rahisi. Mwingine utakuwa unachosha. Lakini kila mara unaporudia kusema “Mama/Baba yupo hapa,” unamjengea mtoto wako msingi wa usalama wa kihisia. 

Na hicho ndicho kitamfundisha kulala kwa amani. Siyo ukamilifu. Ni uwepo wetu, upendo wetu, na uaminifu wetu. Na hiyo ni zawadi kubwa zaidi tunayoweza kuwapa.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×