The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Kenya Yaiandikia Serikali ya Tanzania Kuhusu Kushikiliwa kwa Mwanaharakati Boniface Mwangi. Ripoti Zaonesha Mwangi Amerudishwa Kenya Leo Mei 22

Hata hivyo vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti kuwa Mwanaharakati huyo amekwisha fikishwa nchini Kenya kwa barabara leo Mei 22, 2025, huko Ukunda.

subscribe to our newsletter!

Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya imeiandikia Serikali ya Tanzania kuhusu hatma ya Mwanaharakati Boniface Mwangi aliyekamatwa toka Mei 19, 2025, pamoja na mwanasheria kutoka Uganda Agather Atuhaire. Mwangi na Atuhaire wote walifika nchini kwa ajili ya kuhudhuria kwenye kesi ya uhaini ya Tundu Lissu, kiongozi wa  chama kikuu cha upinzani Tanzania, CHADEMA.

“Wizara ingependa kuonesha wasiwasi wake juu ya kukamatwa kwa Boniface Mwangi, raia wa Kenya mwenye pasipoti namba 472892,” inaeleza taarifa hiyo kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya.

“Pamoja na maombi yetu, watendaji wa Serikali ya Kenya hawajaweza kuwasiliana na Mwangi. Wizara ina wasiwasi juu ya afya yake, hasa kutokana na kutokuwa na taarifa zaidi kuhusu kukamatwa kwake,” inaeleza taarifa hiyo iliyoandikwa Kwenda Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania.

Ingawa sio kawaida kwa mawasiliano kati ya Wizara hizi kuwekwa wazi, kwa upande wa Kenya kumekuwa na msukumo mkubwa kutoka kwa wanaharakati, watetezi wa haki, na familia ya Boniface Mwangi kutaka kufahamu mahali alipo Mwangi na hali yake ya kiafya.

SOMA ZAIDI: Waziri Kiongozi Kenya Aunga Mkono Alichosema Rais Samia Juu ya Wanaharakati: ‘Kuna Ukweli’

Taarifa hizi kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya zinakuja ikiwa ni siku mbili toka Waziri Kiongozi wa Kenya, Musalia Mudavadi kuiambia kituo cha televisheni cha Citizen kuwa Balozi wa Kenya aliweza kuwasiliana na Mwangi.

Mke wa Mwangi pamoja na watetezi wa haki za binadamu nchini Kenya walifika nje ya Ubalozi wa Tanzania jana Mei 21, 2025, kuuliza kuhusu taarifa za Mwangi.

“Boniface hutetea haki za watu kila kona ya dunia, sio sawa haki zake kuminywa namna hii. Hii sio sawa, wamuachie huru,” alieleza Njeri Mwangi ambaye ni mke wa Boniface Mwangi akiwa nje ya Ubalozi wa Tanzania.

Katika taarifa yake Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya imekumbusha kuhusu Mkataba wa Kimataifa wa Vienna, hasa juu ya balozi ya nchi husika kuwasiliana na raia wake, ikiwemo haki ya kumtembelea raia wake rumande, gerezani au wakiwa kizuizini.

“Wizara ya Mambo ya Nje na Masuala ya Diaspora inatoa wito kwa serikali ya Tanzania kuwezesha bila kuchelewa, ubalozi wa Kenya kuongea na Mwangi kwa mujibu wa matakwa ya sheria za kimataifa na sheria za mambo ya nje,” ilieleza taarifa kutoka serikali ya Kenya.

Kwa upande mwingine, wanasheria wa Boniface Mwangi wamewasilisha ombi mahakamani kutaka Jeshi la Polisi, Uhamiaji kutoa taarifa za wapi alipo Mwangi, ambapo kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa Mahakamani mnamo Mei 23, 2025.

Hata hivyo vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti kuwa Mwanaharakati huyo amekwisha fikishwa  nchini Kenya kwa barabara leo Mei 22, 2025, na kupatikana huko Ukunda Kenya, eneo karibu na mji mkubwa wa Mombasa, na mpaka wa Tanzania.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×